Posts

Showing posts from 2017

Donald Ngoma kuzikosa mechi za kanda ya ziwa

Image
Ngoma amefanikiwa kufunga magoli 2 katika mechi 5 za Ligi Kuu mpaka sasa.    Kocha wa Yanga,  George Lwandamina atamkosa mshambuliaji wake hatari raia wa Zimbabwe Donald Ngoma, baada ya taarifa ya daktari wa timu hiyo kuthibitisha ukubwa wa tatizo alilokuwa nalo. Lwandamina ameiambia Goal,  kumkosa Ngoma ni lengo kubwa katika safi yake ya ushambuliaji hasa katika mechi ngumu inayowakabili Jumamosi hii dhidi ya Kagera  Sugar. "Ngoma ni mchezaji muhimu kwenye kikosi changu kumkosa ni pengo kubwa ingawa nafuahia kurejea kwa Amissi Tambwe ambaye Naye alikuwa majeruhi tangu kuanzia kwa msimu huu" amesema Lwandamina. Kocha huyo raia wa Zambia amesema taarifa ya daktari Edward Bavu,  imemhuzunisha lakini hawezi kupingana na ukweli uliopo mbele yake. Lwandamina mategemeo yake kwasasa kwenye safi ya ushambuliajo yatabaki kwa Ibrahim Ajibu na Tambwe huku pia akiamini wachezaji Obrey Chirwa na Emmanuel Martini watafanya...

Timu za Ligi Kuu Bara zenye wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram

Image
Yanga: Wanashika nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram, in wafuasi elfu 82  Azam: Waoka Mikate hao wa Dar es salaam, wanajumla ya wafuasi 108,000 kwenye akaunti yao ya Instagram, ana shika nafasi ya pili nyuma ya klabu ya Simba.  Simba: Ndiyo klabu yenye wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram hapa nchini, ina jumla ya wafuasi ya zaidi ya 196,000  Mbeya City: Anazidiwa wafuasi na klabu za Dar es salaam pekee, ana kamata nafasi ya nne baada ya kuwa na wafuasi 64 katika akaunti yake ya Instagram.  Mtibwa Sugar: ana jumla ya wafuasi 38 katika akaunti yake, ana kamata nafasi ya tano kwa klabu zenye wafuasi wengi Instagram.

Cannavaro aipa Yanga ushindi dhidi ya Kagera Sugar

Image
Mabingwa watetezi Yanga Oktoba 14 watakuwa ugenini uwanja wa Kaitaba kucheza na Kagera Sugar na nahodha wake Cannavaro ameahidi ushindi    Nahodha mkuu wa klabu ya Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro, amesema wamejipanga kucheza kwa bidii ili kuweza kushinda mechi yao dhidi ya Kagera Sugar. Cannavaro, ameiambia YOUNGA , wamefanya mazoezi ya kutosha kujiandaa na mechi za kanda ya ziwa na anaamini watashinda kutokana na uimara. “Nashukuru mambo yetu yote yanakwenda vizuri lengo letu ni ushindi na ninamaani hivyo kulingana na matayarisho yetu,” amesmea Cannavaro. Cannavaro ambaye hajaichezea Yanga hata mechi moja amesema hamasa ni kubwa kwenye kambi yao. Nahodha huyo amesema pamoja na ligi kuonekana kuwa mgumu lakini  wamejipanga kufanya kama msimu uliopita. Yanga inashika nafasi ya sita kwenye msimamo ikiwa na pointi 2 ambazo ndiyo wanazo kwasasa baada ya kucheza mechi tano za ligi.

Yanga watamba kurudi na pointi 6 Kanda ya Ziwa

Image
Uongozi wa Yanga umeahidi kurudi na pointi sita katika mechi zao mbili watakazokwenda kucheza kwenye mikoa ya Kagera na Mwanza kuanzia Jumamosi ijayo Mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga wanatarajia kuoandoka Dar es Salaam, Alhamisi kuelekea mkoani Kagera, kwa ajili ya pambano lao la Jumamosi dhidi ya Kagera Sugar. Msemaji wa Yanga Dismas Ten, ameiambia Goal , kikosi chao kinatarajia kuondoka na nyota wake wote kuelekea Kagera na Mwanza, kwa ajili ya mechi hizo ambazo wamepanga kushinda na kurudi na pointi zote sita. “Tunakwenda kucheza mechi mbili dhidi ya Kagera Sugar na Mbao na zote ni mechi ngumu na ukweli tumepania kushinda ndiyo maana tunakwenda mapema tukiwa na kikosi chetu kamili,” amesema Ten. Msemaji huyo amesema wachezaji wao wote wapo sawa na hakuna aliyekuwa majeruhi jambo ambalo linawapa matumaini ya kutimiza kile ambacho wamekikusudia kukifanya kwenye mechi hizo. Msemaji huyo aliyewahi kufanya kazi na klabu ya Mbeya...

LIGI KUU BARA...WACHEZAJI MAHIRI KUPIGA MIPIRA YA ADHABU NDOGO

Image
                       Ibrahim Ajibu |  Amekuwa akifunga magoli ya mipira ya adhabu mara kwa mara tangu akiwa Simba, msimu huu tayari amesha fanya hivyo dhidi ya Njombe Mji                   Thaban Kamusoko |  Tangu ajiunge na Yanga misimu mitatu nyuma amekuwa ndiye mpigaji maalumu wa mipira ya adhabu, Hajawahi kufanya kosa                 Shiza Kichuya |  Amejizolea umaarufu katika kipengele cha kupiga mipira ya adhabu maarufu kama "Kichuya Kona".                   Emmanuel Okwi |  Ni mara ya tatu anarudi kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara, awamu moja Yanga na hii ni ya tatu kwa Simba, msimu huu bado hajaonyesha cheche zake, lakini anak...

NATAKA KUFUNDISHA YANGA

Image
Nahodha wa Yanga Nadiri Haroub amesema hachukii maamuzi ya kocha wake George Lwandamina kumuweka benchi na zaidi anajifunza ili kuja kuwa kocha    Nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema atakapostaafu kucheza soka anataka kusomea ukocha ili kuja kuchukua mikoba ya kocha wake wa sasa George Lwandamina. Cannavaro licha ya kuwa na cheo hicho lakini amekuwa hapati nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kutokana na umri wake kumtupa mkono. “Hata kama sichezi lakini nafurahi kuwa benchi kwasababu najifunza mambo mengi kutoka kwa makocha waliopo na lengo langu baada ya kustaafu kucheza nataka kuja kuifundisha Yanga siku zijazo,” amesema Cannavaro. Nahodha huyo ameiambia YOUNGA AFRICAN ,  hakuna kinachoshindikana katika hilo kwani kwakipindi cha misimu 11, alichoitumikia Yanga ameweza kujifundisha mambo mengi kutoka kwa makocha mbalimbali ambao wamepitia timu hiyo. Mkongwe huyo amesema mipango yake baada ya kustaafu kucheza soka ni kwenda...

AJIBU AANZA KUTIMIZA WAJIBU

Image
        Pamoja na ushindani mkali lakini mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara Yanga ,wameonja ladha ya ushindi kwa kuifunga Njombe Mji    Mshambiliaji wa zamani wa Simba Ibrahim Ajibu leo ameipa pointi tatu klabu yake mpya ya Yanga baada ya kufunga bao pekee lililoipa timu hiyo pointi tatu walipokuwa wanacheza ugenini dhidi ya Njombe Mji ya Ruvuma. Bao hilo limeifanya Yanga kufikisha pointi nne sawa na timu ya Simba, lakini mabingwa hao wapo kwenye nafasi ya tano kwenye msimamo huku Simba wakiongoza ligi hiyo kwa tofauti ya mabao. Ajibu alifunga bao hilo mapema dakika ya 16, akipiga mpira wa adhabu ndogo uliompita kipa wa Njombe Mji David Kisu na mpira kujaa wavuni. Wenyeji Njombe Mji ndio waliouanza mchezo huo kwa kasi lakini baada ya dakika tano walijikuta wakikaribisha mashambulizi ya Yanga kwenye lango lao na kufungwa bao hilo ambalo lilidumu kwa muda wote wa mchezo. Mshambuliaji wa Yanga Donald ...

NATISHA SABABU YA KOCHA WANGU-MSUVA

Image
Msuva amesema kiwango chake bora alichokionyesha  dhidi ya Botswana, kimetokana na juhudi binafsi ambazo amezionyesha tangu kujiunga na Difaal    Mshambuliai wa Difaal El Jadida ya Morocco, Simon Msuva, amesema siri ya kufanya kwake vizuri ni kutokana na mbinu alizopewa na kocha wake Bderrahim Taleb, anayeifundisha timu hiyo aliyojiunga nayo hivi karibuni akitokea Yanga. Msuva ameiambia YOUNGA AFRICAN , kwa muda mfupi alioichezea timu hiyo ameweza kujifunza mengi ikiwemo mbinu za kuwatoroka na mabeki na kufunga mabao kama aliyofunga jana na kuipa ushindi wa mabao 2-0 Tanzania. “Naweza kusema bado kuna mambo mazuri zaidi yanakuja kutoka kwangu kwani huu ndiyo mwanzo hata ligi haijaanza lakini nimekuwa na mwanzo mzuri ambao mpaka sasa miweza kufunga mabao 9 katika mechi 12 za kirafiki nilizocheza,”amesema Msuva. Mshambuliaji huyo wa pembeni pia amemshukuru kocha Salum Mayanga kwa kumuita kwenye kikosichake na kumpa nafasi ya kucheza hata k...

TAMBWE NA CHIRWA KUISUBIRI SIMBA

Image
Kocha wa Yanga George Lwandamina amewaondoa kwenye kikosi chake kitakacho kwenda Kusini wacheza Tambwe na Chirwa ili wapone vizuri majeraha yao    Kocha George Lwandamina wa Yanga amewaondoa wachezaji, Obrey Chirwa na Amissi Tambwe, kwenye kikosi kitakacho kwenda Nyanda za Juu Kusini kwa ajili ya mechi mbili za ligi dhidi ya Njombe Mji na Majimaji FC. Lwandamina ameiambia YOUNGA AFRICAN , kuwa analazimika kuwaacha wachezaji hao ili waweze kupona vizuri na atawatumia kuanzia mchezo dhidi ya Ndanda FC, ambao utapigwa Dar es Salaam Septemba 23 na ule dhdi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa Septemba 30. “Wanakosa fitness ndiyo maana nataka kuwapumzisha ili wafanye mazoezi kwa muda mrefu zaidi lengo ni kuwaanda kwa ajili ya mechi hizo na nyingine ambazo tutakwenda kucheza kanda ya Ziwa kabla ya kupambana na Simba Oktoba 28,”amesema Lwandamina. Kocha huyo raia wa Zambia amesema maandalizi yao yanakwenda vizuri kuhakikisha wanashinda mechi hizo mbili amba...

AZAM FC YAFURAHIA MECHI ZAKE NA YANGA KUPELEKWA CHAMANZI

Image
Mabadiliko ya ratiba mpya ya Ligi Kuu yanaonyesha kuwa mechi zote za Azam FC za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga zitafanyika Uwanja wa Azam Complex.   Klabu ya Azam FC imefuraishwa na taarifa za shirikisho la mpira TFF kuruhusu mechi zao dhidi ya  Simba na Yanga kufanyika kwenye uwanja wao wa Chamanzi. Kwa mara ya kwanza mechi ya Azam na Simba itafanyika katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Jumamosi hii Septemba 9. " Ni furaha tupu ndani ya viunga vya Azam Complex kwenye makao makuu ya Klabu BIngwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuiruhusu timu hiyo kutumia uwanja huo kwa mara ya kwanza kwenye mechi zake za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga. waliandika hivyo kupitia kwenye mtandao wao wa klabu.

SIMBA KUTWAA UBINGWA NI NDOTO ZA ALINACHA

Image
Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Donald Ngoma, amesema hadi kumalizika kwa mzunguko wa kwanza Yanga itakuwa kileleni mwa msimamo wa ligi Kuu ya Tanzania Bara. Ngoma ameiambia YOUNGA AFRICAN, kuwa katika kipindi cha misimu miwili aliyocheza Tanzania anawajua vizuri wapinzani wao Simba hivyo haoni kama kuna tatizo kwa wao kuongoza ligi. “Ninauhakika hadi kumalizika kwa mzunguko wa kwnza Yanga tutakuwa kileleni au tunatofautiana pointi moja au mbili na timu itakayoongoza ligi kutokana na kasi tuliyonayo,” amesema Ngoma. Mshambuliaji huyo amesema siku zote Simba wamekuwa na papara ya kuanza kwa kasi lakini wao wamekuwa wazuri kwenye kumalizia mbio hizo na hatimaye kutwaa ubingwa. Amesema anatambua kuwa msimu huu ni mgumu na wenye ushindani mkubwa lakini haoni kikwazo ambazho kitaweza kuwazuia wasiweze kutwaa ubingwa. Ngoma tayari anabao moja alilofunga kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Lipuli ambapo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

KAMATI IMENITENDEA HAKI...

Image
Kiungo mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa ameachiwa huru na Kamati ya masaa 72 ambayo ipo chini ya Bodo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.    Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia anayekipiga kwenye klabu ya Yanga Obrey Chirwa amesema anafurahi kwa kuachiwa huru na Kamati ya Nidhamu na Sheria ya TFF. Chirwa ameiambia SOKA DUNIANI , Kamati imetenda haki kwani yeye hakuhusika kabisa kwenye tukio lile lakini ni muda wake sasa kujipanga kwa ajili ya kuipigania timu yake kwenye mechi za ligi zinazoendelea. “Nashukuru kuona nimekutwa sina hatia kwasasa najipanga kwa ajili ya kuipigania timu yangu iweze kufanya vizuri kwenye ligi,”amesema Chirwa. Kwa pamoja, wakiwa wachezaji wa Yanga, Chirwa, Kaseke na winga mpya wa Difaa Hassan El- Jadida walidaiwa kumsukuma na kumwangusha refa Ludovic Charles katika mechi namba 236 ya Ligi Kuu iliyokutanisha timu hiyo na wenyeji, Mbao FC walioibuka na ushindi wa 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Hata hivyo, ba...

MRITH WA BOSSOU ATUA JANGWANI

Image
Yanga inamsaka mrithi wa Vincent Bossou, ambaye aligoma kusaini mkataba mpya msimu ulioisha  Kwa mujibu wa gazeti la michezo la Mwanaspoti, Klabu ya Yanga imeanza mipango ya dirisha dogo la usajili baada ya kumvuta,  Kayembe Kanku Fiston kwa ajili ya majaribio,  akitokea klabu ya SM Sanga Balende yenye makazi yake nje ya Jiji la Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Beki huyo ameletwa na kiungo mpya wa Yanga, Papy Tshishimbi, Mcongo huyo amewahakikishia Yanga kwamba mchezaji huyo ni fundi na wataona yake kwenye majaribio ambayo atayaanza baada ya kocha kurejea. Amewaambia viongozi kuwa akishirikiana na kina Kelvin Yondani, Yanga itakuwa imara sana nyuma. Fiston atajaribiwa kwa wiki mbili ambapo endapo uwezo wake utakubalika, atasaini mkataba wa awali na Yanga na kurejea klabuni kwake. Imeelezwa kuwa atarejea tena nchini kuja kujiunga na mabingwa watetezi hao wa Ligi Kuu Bara wakati wa usajili wa dirisha dogo la usajili likalaofunguliwa Novem...

KUNA PRESHA KUBWA KUCHEZA YANGA KULIKO AZAM

Image
Hivi karibuni Gadiel, alijiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Azam ambako alianzia maisha ya soka la ushindani.    BEKI mpya wa Yanga Gadiel Michael, amesema kuna tofauti kubwa kucheza Yanga na klabu nyingine ndogo ambazo hazina presha kama ilivyokuwa Azam FC. Gadiel, amesema maisha ya Yanga ni mazuri lakini kitu kikubwa kinacho mzingua ni presha ya mashabiki ambao kila mechi wanahitaji mchezaji acheze vizuri na timu ipate ushindi. “Kiukweli nimepata mapokezi mazuri kwa wachezaji na hata benchi la ufundi ispokuwa presha ni kubwa kuliko umri wangu tofauti na ilivyokuwa Azam, ingawa nashukuru nifurahi kuona watu wanaikubali kazi yangu,”amesema Gadiel. Beki huyo amesema kitu cha msingi kwake ni kuendelea kucheza kwa kujituma ili kubaki kwenye kikosi cha kwanza vinginevyo anaweza kusota benchi kwani hata msaidizi wake Hajji Mwinyi ni mchezaji mzuri na anaukubali uwezo aliokuwa nao. Amesema atajitahidi kupambana bila uoga ili kuwa...

LWANDAMINA AENDA KWAO ZAMBIA

Image
Kocha wa Yanga George Lwandamina amerudi kwao Zambia leo baada ya kufiwa na mzazi wake wa kiume na atarudi nchini baada ya msiba kwisha    Kocha wa klabu ya Yanga, George Lwandamina ameondoka Dar es Salaam kurudi kwao Zambia, kuhudhiria mazishi ya baba yake mzazi, aliyefariki dunia jana baada ya kusumbuliwa na maradhi ya Kiharusi. Lwandamina ameiambia Goal, atakuwa huko hadi shuhuli za msiba zitakapo malizika ndipo atarudi Dar es Salaam kuendelea na kazi yake ya kukinoa kikosi cha Yanga.  “Nakwenda nyumbani kwenye msiba wa Baba yangu baada ya kumaliza msiba nitarudi kazi kwa ajili ya kuiongoza Yanga kwenye michuano inayotukabili ya ligi ,”amesema Lwandamina. Kocha huyo amesema baada ya yeye kuondoka majukumu yote ya timu amemuachia msaidizi wake Shedrack Nsajigwa pamoja akiamini anaweza kuwasimamia vizuri. Amesema anatambua presha iliyopo baada ya kuanza na sare kwenye mechi yao ya kwanza msimu huu hivyo wanajipanga kuhakikisha wanafanya...

YANGA BINGWA MSIMU HUU ANENA MSUVA

Image
Simon Msuva ana amini kuwa klabu ya Yanga inayo nafasi ya kutetea ubingwa kwa mara ya nne mfululizo    Klabu ya Yanga itakuwa mabingwa wa Ligi Kuu kwa mara nyingine tena kutokana wachezaji wengi kukaa kwa muda mrefu pamoja,  kadhalika na aina ya usajili bora walioufanya msimu huu kwa mujibu wa winga wazamani wa Yanga, Simon Msuva. Msuva amejiunga na klabu ya Difaa el Jadida ya nchini Morocco, kwa dau linalokadiliwa dola 160,000 lilitumika kumg'oa Yanga. “Nimefuatilia mechi za mwanzo za ligi ya Tanzania na nimesikia Simba wameanza kwa kushinda 7-0, wakati timu yangu ya zamani ya Yanga ikitoka sare, watu wengi wanasema Simba itakuwa bingwa, lakini binafsi naona Yanga ndiyo yenye nafasi ya kufanya hivyo tena.alisema hivyo wakati akihojiwa na mtandao wa Salehe Jembe. “Nasema hivyo kwa sababu ukiangalia kweli zote zimefanya usajili wa maana, lakini Yanga ina wachezaji wengi waliokaa pamoja na kuzoeana tofauti na Simba yenye sura nyingi mpya. ...

KAMUSOKO SI WA KAWAIDA;;;;HAJI MANARA

Image
Kwa mujibu wa Haji Manara ana amini kwa uwezo mkubwa alionao Thabani Kamusoko si wakucheza hapa    Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amemvulia kofia kiungo wa klabu ya Yanga Mzimbabwe, Thabani Kamusoko kutokana na umahiri wake mkubwa wa kusukuma kabumbu. Thabani Kamusoko alijiunga na Yanga misimu miwili nyuma akitokea klabu ya FC Platnumz ya nchini Zimbabwe. Katika misimu mitatu Jangwani, Kamusoko amefanikiwa kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu Bara, moja la FA na Ngao ya Jamii, kadhalika na kuiwezesha Yanga kucheza hatua ya makundi, kombe la Shirikisho Afrika misimu miwili nyuma chini ya mwalimu, Hans Van Pluijm. Akitumia akaunti yake ya Instagram, Haji Manara amesema kiungo huyo si wakucheza nchini hapa kutokana na uwezo wake mkubwa "Huwa sifichi mahaba yangu kwa mchezaji anayenivutia uwanjani, hata kama anachezea Klabu nisiyoishabikia, Scara kamusoko hapewi heshma anayostahili nchi hii, ni level ya kucheza Europe "

SARE KITU GANI? SUBIRI MZIKI WETU

Image
Kocha wa Yanga amesisitiza kuwa Yanga bado ipo imara na malengo hayajavurugika ingawa Lipuli walikamia mchezo  Kocha wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara George Lwandamina amesema sare waliyoipata jana dhidi ya Lipuli FC haijawavurugia mipango ya kutetea ubingwa wao. Lwandamina ameiambia SOKA DUNIANI timu yake ilicheza vizuri lakini wapinzani wao waliziba njia walizopanga kuzitumia ndiyo mana wakapata sare. "Tulicheza vizuri wachezaji walijituma lakini tukashindwa kutumia nafasi tulizozipata lakini hilo halitutoi kwenye mbio za ubingwa kwasababu ndiyo mchezo wa kwanza bado tuna michezo mingi," amesema. Mzambia huyo amesema kuwa wapinzani wao waliingia kwa kuwakamia na kuwachezea rafu baadhi ya wachezaji wake kitu ambacho kilivuruga mipango yao. Amesema wanetambua mapungufu yao na wanakwenda kuyafanyia kazi akiamini kwamba mchezo unaofuata dhidi ya Njombe Mji watarekebisha na kupata matokeo. Yanga ilianza vibaya harakati za kutetea ubingwa...

YONDANI AULA TAIFA STARS

Image
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Salum Mayanga amemrudisha beki Kelvin Yondani kwenye kikosi cha Taifa Stars ambacho kitapambana na Botswana Sap 2    Kocha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Salum Mayanga, ameita kikosi cha wachezi 21, kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Botswana. Mayanga ameiambia YOUNGA AFRICAN , kikosi hicho kitaingia kambini kesho kujiandaa na mchezo huo ambao ni maandalizi kwa ajili ya kujiandaa na mechi za kufuzu fainali ya Mataifa ya Afrika. “Timeita kikosi kulingana na kiwango cha mchezaji pamoja na nidhamu yake kwani naamini wachezaji hao wataitikia wito mapema na tutafanya vizuri kwenye mchezo huo,” amesema Mayanga. Katika kikosi hicho alichokitaja leo Mayanga amemrejesha beki mkongwe wa Yanga, Kevin Yondan Mayanga amesema kwamba kwa sababu ya majeruhi hajawaita kipa Said Mohammed ‘Ndunda’ na mshambuliaji John Raphael Bocco, wote wa Simba. Mayanga amesema kwa sababu kama hizo p...

LIPULI LAZIMA IZIKWE

Image
Uzoefu wa Yanga unaweza kuupa mwanzo mzuri na kuweka matumaini ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, msimu huu    Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania bara Yanga LEO wanashuka uwanjani kuwakabili Lipuli FC,  ya Iringa katika pambano ambalo limepangwa kupigwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga itawakosa nyota wake Obrey Chirwa na Pius Buswita kutokana na kesi tofauti ambapo Buswita amesimamishwa mwaka mmoja baada ya kubainika kusaini mara mbili Simba na Yanga. Chirwa licha ya kuwa ni majeruhi lakini pia, alisimamishwa na Kamati ya usimamizi ya uendeshaji Bodi ya ligi ile ya masaa 72 ya msimu uliopita baada ya kumpiga mwamuzi Ludovic Charles katika mchezo wa kumaliza msimu dhidi ya Mbao FC hivyo, anasubiri suala lake kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Yanga imekuwa haitabiriki katika mechi zake za mwanzo kuna wakati huanza vibaya na wakati mwingine hu...

NIYONZIMA NA AJIBU...NANI ATASHINDA?

Pambano lililosubiriwa kwa siku nyingi limefika, ni Simba dhidi ya Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii, Niyonzima na Ajibu wakikabili timu zao za kale    Miamba ya soka Tanzania Yanga na Simba inakutana kesho Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa Ngao ya Jamii ambao unaashiria kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom. Presha imekuwa kubwa kwa pande zote mbili, huku Simba wakiwa na matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo kutokana na usajili ambao wameufanya msimu huu kwa kusajili nyota wenye majina makubwa. Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa ni Februari mwaka huu, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, kwahiyo usajili walioufanya msimu huu pamoja na ushindi walioupata mwisho kumewajengea imani mashabiki wa Simba wakiamini rekodi hiyo itaendelea tena kesho. Kuelekea mchezo huo Yanga wameendelea kujifua kwa kutumia nyota waliosajili kipindi hiki cha usajili ingawa mashabiki wao wameonyesha hofu kutokana na ...

NGOMA APANIA KUIFUNGA SIMBA KESHO

Image
Mshambuliaji wakimataifa wa Yanga Donald Ngoma amesema atahakikisha anaifungia bao timu yake kesho wakati ikipambana na Simba uwanja wa Taifa Dar  Mshambuliaji wa Yanga raia wa Zimbabwe Donald Ngoma, amesema yupo fiti kwa ajili ya kuwaangamiza Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utapigwa kesho uwanja wa Taifa. Ngoma ameiambia YOUNGA AFRICAN , haoni ugumu wowote kuelekea mchezo huo na hiyo ni kutokana na kupona majeruhi yaliyomsumbua kwa muda mrefu na ubora wa kikosi chao ulivyo. “Bado sijaona beki wa Simba ambaye anaweza kunizuia kwanza nina hasira nao sana baada ya kukosa mechi mbili za msimu uliopita imeniuma sana walivyotufunga na nisingependa matokeo yale yajirudie tena,”amesema Ngoma. Mshambuliaji huyo aliyeongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga, amesema anataka kurudisha heshima Yanga kama ilivyokuwa wakati wa nyuma ambapo waliweza kutamba kwa kuzifunga timu zote kubwa nchini. Amesema ili kuthibitisha kuwa wao ni timu kubw...

WACHEZAJI WA KUCHUNGWA SIMBA VS YANGA

Image
Young African inakuletea wachezaji wa kuchungwa kuelekea mchezo wa Yanga na Simba Simba  na Yanga zitashuka dimbani siku ya Jumatano, Agosti 23 uwanja wa Taifa Dar es salaam kwa ajili ya mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii Ukiachana na historia ya pambano hilo, pia ukubwa wa mtanange huo unatokana na nyota wapya waliopo kwenye klabu zote mbili Timu zote mbili zinatarajiwa kuwakosa nyota wake muhimu wa kikosi cha kwanza kutokana na majeraha wanayouguza, Kakolanya, Mwashiuya na Chirwa kwa upande wa Yanga wanatarajiwa kukosekana huku Bocco, Kapombe, Mohammed Hussein kwa upande wa Simba wakiwa na asilimia kubwa ya kuukosa mchezo huo. YOUNG AFRICAN  inakuletea wachezaji wa kuchungwa kuelekea mchezo wa Yanga na Simba Amissi Tambwe - Yanga Amekuwa na rekodi nzuri ya kuifunga Simba tangu ajiunge na Yanga misimu 3 nyuma, Mrundi huyo anaitaji ulinzi mkubwa kumzuia hasa kwa mipira ya hewani, kama kona na krosi Shiza Kichuya - Simba Ni mwi...

TAMBWE"NIMEMISSI KUIFUNGA SIMBA"

Image
Tambwe amefanikiwa kuifunga Simba magoli matatu kwenye mechi tano Mshambuliaji wa Yanga raia wa Burundi, Amissi Tambwe amesema ana hamu ya kuitungua klabu ya Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii siku ya Jumatano Akizungumza na gazeti la michezo la Champion, Mrundi huyo amesema kuwa ana hamu kubwa sana ya kuona akizifumania nyavu siku hiyo kwani amemisi kuifunga timu hiyo. “Namshukuru Mungu hivi sasa nipo fiti na ninaendelea vizuri na maandalizi yangu kuelekea mchezo huo baada ya kupona goti lililokuwa likinisumbua hivi karibuni. “Ninamshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema na nipo tayari kwa ajili ya mechi ya Jumatano dhidi ya Simba, kwani nimemisi sana kuifunga jambo ambalo linanifanya nijisikie vibaya kila wakati. “Endapo nitapata nafasi ya kuanza hiyo Jumatano dhidi ya Simba, nitahakikisha napambana vilivyo ili niweze kuzifumania nyavu roho yangu itulie kwani nataka nizidi kuandika rekodi ya kuifunga mara nyingi,” alisema Tambwe.

CHIRWA KUIKOSA SIMBA NGAO YA JAMII

Image
Shirikisho la soka Tanzania TFF, limemuengua Obrey Chirwa, kwenye kikosi cha Yanga kitakacho ikabili Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii  Yanga itamkosa mshambuliaji wake wa pembeni katika pambano la Ngao ya Jamii Jumatano Mzambia Obrey Chirwa kutokana na adhabu ya kadi ya kumwangusha refa katika mchezo wa ligi ya Vodacom dhidi ya Mbao FC msimu uliopita. Msemaji wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, Alfred Lucas ameiambia Soka Duniani, adhabu ya Chirwa inatumika pande zote mbili kwenye mechi ya ligi pamoja na michuano ya FA. “Tunawatahadharisha Yanga wasije kumtumia Chirwa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii Jumotano dhidi ya Simba kwasababu anatumikia adhabu aliyopata kwenye mchezo wa mwisho wa ligi ya Vodacom msimu uliopita,”amesema Lucas. Lucas amesema Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji bado haijaketi na kutoa maamuzi hivyo mchezaji huyo ataendelea kuwa nje hadi hapo hukumu yake itakapotoka. Amesema kama kufikia Jumamosi Kamati hiyo itakuwa haijakutana na ...

KIUNGNO MWENGINE WA RASTA ASINI

Image
                                                            WAKATI kiungo rasta, Tshishimbi Kabamba ‘Papii’ akisaini mkataba wa miaka miwili kuitumia Yanga, mabosi wa klabu hiyo wamefanya kitu kingine cha maana baada ya kumalizana na kiungo mwingine fundi. Yanga imemsainisha kiungo Raphael Daud kutoka Mbeya City tayari kuitumikia klabu hiyo na leo Ijumaa timu inatarajiwa kutua kambini mjini Morogoro kuungana na wachezaji wenzao kwa maandalizi ya msimu mpya wa mashindano. Habari kutoka kwa mabosi wa Yanga, ni kwamba Rafael alisainishwa mkataba huo juzi Jumatano, lakini waliamua kufanya siri kwa sababu kuna mambo hawajamalizana na klabu yake ya City. “Rasta amesaini tayari kuanza kuitumikia Yanga, lakini pia tumemalizana na kiungo Rafael Daud ambaye tulishaanza mazungumzo naye mapema, lakini ikawa bado kusaini ...

WASAJILIWA WA YANGA NI WA KIMATAIFA ZAIDI.

Image
                    Mwenyekıtı wa kamati ya usajili wa tımu ya yanga HUSSENI NYIKA amesema kuwa usajılı wa tımu yake nı wakımataıfa kulıngana na wachezajı wao walıowasajili kuwa ni wa vıwango vya kımataifa amesema amesajıli madhubutı ıli kujua wanafnya vrzri kımataifa.                                                                Waliosajıriwa nı Ibrahimu Ajibu. Abdallah Shaıbu. Ibrahımu Yahaya. Donald Ngoma. Thabanı kamusoko. Nyıka amesema wamefıkia usajili wao kwa asilimia 95%. Pamoja na hayo amesema kuwa wapochezajı walio mwagwa kuwa ni Raphel Daudai Mbeya city.                                                             ...

''OJ'' OSCAR JOSHUA CINA KINYONGO NA YANGA

Image
 Aliekuwa beki  kushoto Oscar Joshua mwenye mwılı kaa Jumba ameondoka Yanga akıwa hana kınyongo na tımu .Amesema ataendlea kuıkumbuka Yanga katika maisha kwanı imeweza kumsaidia kımaisha kufikia hapo alipo cına kinyongo na yanga kwanı maısha ndıvo yalivyo.  Mchezajı huyo amesaema kuwa yanga kuachwa kwakwe katıka msımuu huu hakutamnfnya aache kuıkumbuka yanga kwanı ımemfanya aweze kucheza  kıımataıfa na taıfa kwa ujumla xaxa kanajıpanga kuibuka kiivıngıne.        “Yanga, ina watu tofauti na wenye kazi tofauti, nilikuwa makini kutumia nafasi hizo ili kujifunza mengi yenye faida kwa maisha yangu, sitaacha kuishukuru na kuachwa kwangu hakuwezi kujenga uhasama nao,” alisema Oscar ‘OJ’  Ijulikane kuwa waliosajiriwa yanga wanahıtajı kujıtuma.

MAZOEZI YA YANGA YAANZA WAKIWA NA NYOTA WAAPYA

Image
                                 Dar es Salaam.Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imeanza mazoezi ya uwanjani, ikiwa na nyota wake wapya wakiwamo Mkameruni, Fernando Bongyang na Mnigeria Henry Tony Okoh walipiga mpira mwingi, huku Kiberenge Burhan, Yahya Akilimali akifunika zaidi. Mazoezi hayo yalifanyika jana asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam chini ya Kocha George Lwandamina na wasaidizi wake, ambapo asilimia kubwa ya wachezaji waliosajili na timu hiyo na wale wa zamani walishiriki. Kipa Youthe Rostand, Ibrahim Ajib, Akilimali na nyota hao wa kigeni wanaowania nafasi moja iliyosalia walionyesha uwezo wao, japo kiungo rasta kutoka Swaziland, Tshishimbi Kabamba 'Papii' hakuwepo kabisa uwanjani hapo. Kocha Lwandamina alisema ameanza vizuri kuwaona vijana wake na anaimani ataendelea kuwasoma kadri wakiendelea kujifua baada ya kutumia wiki mbili na ushei kwenye ma...

KESSY APATA PRESSURE YA MAJINA MAKUBWA KIKOSINI ''SAPRAIZID''

Image
                       BEKI wa Yanga, Hassan Kessy, ametamka kauli ya kishujaa kwamba mechi ya Ngao ya Jamii itakayopigwa Agosti 23 kati yao na Simba ni nyepesi sana, ila kinacholeta presha ni sapraizi ya majina makubwa ya mastaa waliosajili kikosini. Kessy aliyenyakuliwa kitatanishi toka Simba, alisema ujio wa nyota wapya Yanga umeongeza presha kikosini, lakini hiyo ni dalili njema za Yanga kutisha msimu huu. “Kuna tofauti ya ugumu wa mechi na majina makubwa ya wachezaji, mfano mzuri ni uhamisho wa Ibrahim Ajibu kutoka Simba kuja Yanga, hilo linaibua presha kwa mashabiki kuona kama kuna kitu cha ajabu kinakuja wakati soka ni lile lile,” alisema Kessy. Kuhusu mechi hiyo ya Ngao ya Jamii, alisema haoni cha ajabu katika mechi hiyo zaidi ya mchezaji kuzingatia majukumu yake uwanjani na kutovunja sheria za soka kwa maana ya mashabiki kupata burudani inayotakiwa. “Mtu kama Emmanuel Okwi ni mchezaji gani asiyemjua...

MRITHI SAHIHI WA CHUJI APATIKANA YANGA

Image
Hakuna shaka juu ya hilo.Athuman Idd Chuji alikuwa mchezaji mahiri enzi zake.Akicheza kama kiungo mkabaji,alionyesha uwezo wake na kuwa tishio kwa timu pinzania,Si hapa nchini tu bali pia aliogopwa na kusifiwa hadi nje ya nchi, Lakini tangu alipoondoka yanga,Timu hiyo imeshindwa kumpata mrithi wa kuchukua nafasi yake.Wamejaribiwa wengi lakini hakuna aliyeonyesha au kuukaribia uwezo wa Chuji. Anaitwa Papi Kabamba Tshishimbi .Alikuwa mchezaji wa Mbabane Swallows na alikuja Tanzania kwa mara ya kwanza na timu yake kuvaana na Azam kwenye mchezo wa kwanza wa mtoano wa Kombe la shirikisho.Kiwango chake kilimvutia kocha George Lwandamina na akaamua kumuwekea mashushushu wa kujua ni nani hasa mchezaji huyu.Lwandamina mwenyewe alifika hadi Swaziland kumshuhudia mchezaji huyu katika moja ya mechi alizocheza akiwa na Mbabane Swallows...akaridhika nae. Ni jana tu ,jamaa huyu akatia timu Tanzania kimya kimya na kuanza mazungumzo na uongozi wa Yanga,Mda si mrefu atatambulishwa na kwa ai...

:DOCTOR; SALVATORY EDWARD AENDLEA KUDUMISHA UMOJA NA USHIRIKIANO YANGA.

Image
                                        Kungo mshambulıajı wa Tımu ya Yanga Salvatoyr Edward DOCTOR aendlea kuudımısha umoja na ushırıkaıno kwa vıjana wake alokuwa anawafundısha akıwa kocha wa Yanga . Salvatory kaıchezea yanga mwaka 1990 na kupata mafunıkıo hadı mwaka 2000. Ameendlea kuwapokea vıjana hao na kuwapa nafası amewaongoza vıjana wake jana kucheza mechı ya kırafıkı ya Lıpulı FC kwenye uwanja wa Karume.                   kocha huyo amesema mbalı na kuwapeleka vıjana hao kwenye mechı tofautı tofautı pıa anaendlea kuwauza kweny tımu kubwa ılı waje wacheze kweny lıgıı kuu bara.                Lıpulı fc ınatarajıwa kukarıbıshwa kwnye msımuu huu wa lıgı kuu Tanzanıa Bara 2017/ 2018 na kuaanza kucheza na bıngwa mtetezı Yanga wa lıgıı kuu agostı 27.

KICHUYA HADI KIELEWEKE MIMI NA YANGA

Image
                                                                                    MASHABIKI na wachezaji wa Yanga, huenda bado wanaendelea kumuota Shiza Kichuya kwa jinsi mabao yake mawili yalivyowakata maini katika mechi ya watani msimu uliopita, lakini kama wanadhani watapumua, wamsikie anachokisema. Kichuya aliyesajiliwa Simba kutoka Mtibwa Sugar, ndiye aliyefunga bao la kusawazisha katika mechi iliyojaa utata ya Oktoba Mosi, 2016 kabla ya kufunga bao la ushindi mechi ya marudiano na kuwazima kabisa Yanga, alisema yupo tayari kufanya yake. Winga huyo aliyepo timu ya taifa, Taifa Stars, ambayo kesho Jumamosi itashuka Uwanja wa Amahoro mjini Kigali kucheza mechi ya marudiano ya kufuzu fainali za Chan 2018 dhidi ya wenyeji Rwanda, alisema Yanga haimpi shida kwa vile ...

JEERY MURO AJITOA YANGA

Image
                                                  Aliyekuwa msemaji mkuu wa klabu yanga amesema kuwa Yang ilikufanikiwa katika utendaji ndani ya uongozi wa mabingwa hao wa kihistoria ni lazima kuangalia ni nani anakuletea ushauri. Muro ameyasema hayo ikiwa ni sikuchache tu zimepita tangu Yanga imtangaze msemaji mpya wa timu hiyo, Dismass Ten aliyochukua nafasi yake. “Yanga kuna majungu watu wanapenda wafanye vitu vyao, kuna wanafiki ambao watakwambia ufanye hiki ukikifanya unaingia chaka. “Wapo Yanga SC watu wenye msaada wa kweli, wazuri sana, wenye akili na wenye mapenzi ya kweli kuhakikisha Yanga inakuwa kama    watu wote hao wapo Yanga. “Unachotakiwa kufanya ni kufungua macho kuangalia ni nani anakuletea ushauri, maana kuna mwingine anakuletea ushauri wakati yeye kashindwa kuongoza nyumba yake kaachana na mkewe ,hajali wa...

SIMBA YASAJILI WALINZI KUMI NA NNE (14) KUMZUIA AJIBU

Image
                                         ;KIBERENGE AFURAHI KUCHEZA NA AJIBU            Jana mchana mabosi wa Yanga walimalizana na Burhan Yahya Akilimali aliyedakwa juu kwa juu wakati akiwania kusajiliwa Lipuli na kumsainisha mkataba wa miaka miwili. Yahya anayekwenda kwa jina la utani la Kiberenge kutokana na kasi aliyonayo, ametua Jangwani kuchukua nafasi ya Simon Msuva anayejiandaa kutimkia Morocco na amesema anajisikia furaha kutua timu kubwa yenye nyota kama Ajibu, Tambwe na Ngoma na kuahidi kutowaangusha.                                                                                               ...

FURAHA YANGA YAMPATA KAMUSOKO NA KAMBWILI KIPA WA SERENGETI BOY.

Image
                                                                    Klabu ya Yanga imemsainisha mkataba mpya wa miaka miwili kiungo Mzimbabwe, Thaban Kamusoko huku pia ikimsajili kipa wa Serengeti Boys, Ramadhani Kabwili. Taarifa iliyotolewa na Yanga kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika ni kwamba Kamusoko ameongeza mkataba huo baada ya kufikia makubaliano ya mambo kadhaa. Katika kuimarisha lango lao, Yanga pia imefanya usajili wa Kabwili ambaye alikuwa na Serengeti Boys katika michuano ya Vijana Afrika mwaka huu nchini Gabon. Usajili umeifanya Yanga kukamilisha usajili wa nyota wanne wapya ambapo awali ilimsainisha kipa wa African Lyon, Youthe Rostand, beki Abdallah Shaibu pamoja na mshambuliaji Ibrahim Ajib.

WAKILII DAMASI NDUMARO YAFUTIWA KESI NA TFF

Image
                               Shirikisho la soka nchini Tanzania  (TFF)  limetangaza kumfutia kifungo cha kutojihusisha na masuala ya soka wakili   Damas Ndumaro   ambaye alifungiwa kwa muda wa miaka saba. Maamuzi hayo yamechukuliwa na Kamati ya rufaa ya TFF    chini ya mwenyekiti wake, Rahim Shaban Zuberi ambaye ndiye aliyetangaza maamuzi hayo kwenye ofisi za TFF zilizopo Karume jijini Dar es Salaam, leo Jumatano. Hadi anafikia hatua ya kufunguliwa, Ndumbaro alikuwa ametumikia adhabu yake kwa muda wa miaka miwili na nusu. Katika maelezo yake, Zuberi amesema Ndumbaro hakupata nafasi ya kujitetea na kuna badhi ya mambo hayakuzingatia usawa wakati akifungiwa.