KIUNGNO MWENGINE WA RASTA ASINI
WAKATI kiungo rasta, Tshishimbi Kabamba ‘Papii’ akisaini mkataba wa miaka miwili kuitumia Yanga, mabosi wa klabu hiyo wamefanya kitu kingine cha maana baada ya kumalizana na kiungo mwingine fundi. Yanga imemsainisha kiungo Raphael Daud kutoka Mbeya City tayari kuitumikia klabu hiyo na leo Ijumaa timu inatarajiwa kutua kambini mjini Morogoro kuungana na wachezaji wenzao kwa maandalizi ya msimu mpya wa mashindano. Habari kutoka kwa mabosi wa Yanga, ni kwamba Rafael alisainishwa mkataba huo juzi Jumatano, lakini waliamua kufanya siri kwa sababu kuna mambo hawajamalizana na klabu yake ya City. “Rasta amesaini tayari kuanza kuitumikia Yanga, lakini pia tumemalizana na kiungo Rafael Daud ambaye tulishaanza mazungumzo naye mapema, lakini ikawa bado kusaini ...