JEERY MURO AJITOA YANGA


   
  
                                           Aliyekuwa msemaji mkuu wa klabu yanga amesema kuwa Yang ilikufanikiwa katika utendaji ndani ya uongozi wa mabingwa hao wa kihistoria ni lazima kuangalia ni nani anakuletea ushauri.
Muro ameyasema hayo ikiwa ni sikuchache tu zimepita tangu Yanga imtangaze msemaji mpya wa timu hiyo, Dismass Ten aliyochukua nafasi yake.

“Yanga kuna majungu watu wanapenda wafanye vitu vyao, kuna wanafiki ambao watakwambia ufanye hiki ukikifanya unaingia chaka.
“Wapo Yanga SC watu wenye msaada wa kweli, wazuri sana, wenye akili na wenye mapenzi ya kweli kuhakikisha Yanga inakuwa kama  watu wote hao wapo Yanga.

“Unachotakiwa kufanya ni kufungua macho kuangalia ni nani anakuletea ushauri, maana kuna mwingine anakuletea ushauri wakati yeye kashindwa kuongoza nyumba yake kaachana na mkewe ,hajali watoto wake yeye mwenyewe kufua nguo hafui nguo maisha yake yamemshinda,” alisema Jerry Muro aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo.
Mungu anasema unapojipenda nafsi yako wewe mpende na jirani, kaka kama MTU kashindwa kuendesha familia yake kamwe hawezi kuendesha Yanga”. Muro ameyasema hayo kupitia chombo cha habari cha UFM radio.


Comments

Popular posts from this blog

SIMBA ILIVYONUSURIKA KUSHUKA DARAJA MWAKA 1989

TUJIKUMBUSHE MECHI KALI KATI YA YANGA NA SIMBA NYAMAGANA 1974?

JINSI YANGA ILIVYOIADHIBU SIMBA MWAKA 1994