SIMBA KUTWAA UBINGWA NI NDOTO ZA ALINACHA
Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Donald Ngoma, amesema hadi kumalizika kwa mzunguko wa kwanza Yanga itakuwa kileleni mwa msimamo wa ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Ngoma ameiambia YOUNGA AFRICAN, kuwa katika kipindi cha misimu miwili aliyocheza Tanzania anawajua vizuri wapinzani wao Simba hivyo haoni kama kuna tatizo kwa wao kuongoza ligi.
“Ninauhakika hadi kumalizika kwa mzunguko wa kwnza Yanga tutakuwa kileleni au tunatofautiana pointi moja au mbili na timu itakayoongoza ligi kutokana na kasi tuliyonayo,” amesema Ngoma.
Mshambuliaji huyo amesema siku zote Simba wamekuwa na papara ya kuanza kwa kasi lakini wao wamekuwa wazuri kwenye kumalizia mbio hizo na hatimaye kutwaa ubingwa.
Amesema anatambua kuwa msimu huu ni mgumu na wenye ushindani mkubwa lakini haoni kikwazo ambazho kitaweza kuwazuia wasiweze kutwaa ubingwa.
Ngoma tayari anabao moja alilofunga kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Lipuli ambapo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Comments
Post a Comment