WACHEZAJI WA KUCHUNGWA SIMBA VS YANGA

Young African inakuletea wachezaji wa kuchungwa kuelekea mchezo wa Yanga na Simba
Simba  na Yanga zitashuka dimbani siku ya Jumatano, Agosti 23 uwanja wa Taifa Dar es salaam kwa ajili ya mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii

Ukiachana na historia ya pambano hilo, pia ukubwa wa mtanange huo unatokana na nyota wapya waliopo kwenye klabu zote mbili

Timu zote mbili zinatarajiwa kuwakosa nyota wake muhimu wa kikosi cha kwanza kutokana na majeraha wanayouguza, Kakolanya, Mwashiuya na Chirwa kwa upande wa Yanga wanatarajiwa kukosekana huku Bocco, Kapombe, Mohammed Hussein kwa upande wa Simba wakiwa na asilimia kubwa ya kuukosa mchezo huo.

YOUNG AFRICAN  inakuletea wachezaji wa kuchungwa kuelekea mchezo wa Yanga na Simba

Amissi Tambwe - Yanga

Amekuwa na rekodi nzuri ya kuifunga Simba tangu ajiunge na Yanga misimu 3 nyuma, Mrundi huyo anaitaji ulinzi mkubwa kumzuia hasa kwa mipira ya hewani, kama kona na krosi

Shiza Kichuya - Simba

Ni mwiba kwa upande wa Yanga siku ya Jumatano, mechi mbili za mwisho winga huyo aliibuka shujaa, safu ya ulinzi ya Yanga inaitaji umakini mkubwa na kutoruhusu kufanya faulo maeneo ya karibu kwani, Kichuya ni mpigaji wa mipra ya adhabu

Donald Ngoma - Yanga

Ni mshambuliaji mwenye kasi, nguvu na jicho la goli, pia ni mzuri kwenye mashambulizi ya kushutukiza, ana tazamiwa kuwa mwiba kwa Simba kama asipowekewa ulinzi dhabiti wa kumzuia

Emmanuel Okwi - Simba

Okwi ni mchezaji hatari sana kasi yake, krosi murua na umakini wa kufunga amekuwa akiwapa tabu mabeki wengi hivyo safu ya ulinzi ya Yanga inaitaji umakini wa kumdhibiti.

Thabani Kamusoko -- Yanga

Ndiye kiunganishi wa timu ya Yanga, kuanzia safu ya ulinzi hadi ushambuliaji, hatakiwi kuwa huru kufanya anachotaka kwani ndiye mwenye mipango yote ya klabu ya Yanga

Haruna Niyonzima - Simba

Amejiunga na Simba akitokea Yanga, Harruna anatazamiwa kuwa mwiba kwa upande wa Yanga kama asipowekewa ulinzi mkali, ni mchezaji mbunifu mwenye uwezo wa kufunga, na kutengeneza nafasi kwa washambuliaji

Ibrahim Ajibu - Yanga

Siyo mshambuliaji wa kupewa nafasi muda wote, Ajibu ni mmoja wa nyota wachache kwenye Ligi Kuu wenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira kutokana na ubunifu wake mkubwa

Mzamiru Yassin - Simba

Ni mchezaji ambaye atamkwi sana, ila ni mmoja wa nyota wa kuangaliwa sana kwani mechi nyingi ngumu kwa upande wa Simba amekuwa ndiye msaada mkubwa sana

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA ILIVYONUSURIKA KUSHUKA DARAJA MWAKA 1989

TUJIKUMBUSHE MECHI KALI KATI YA YANGA NA SIMBA NYAMAGANA 1974?

JINSI YANGA ILIVYOIADHIBU SIMBA MWAKA 1994