MRITH WA BOSSOU ATUA JANGWANI


Yanga inamsaka mrithi wa Vincent Bossou, ambaye aligoma kusaini mkataba mpya msimu ulioisha 
Kwa mujibu wa gazeti la michezo la Mwanaspoti, Klabu ya Yanga imeanza mipango ya dirisha dogo la usajili baada ya kumvuta,  Kayembe Kanku Fiston kwa ajili ya majaribio,  akitokea klabu ya SM Sanga Balende yenye makazi yake nje ya Jiji la Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Beki huyo ameletwa na kiungo mpya wa Yanga, Papy Tshishimbi, Mcongo huyo amewahakikishia Yanga kwamba mchezaji huyo ni fundi na wataona yake kwenye majaribio ambayo atayaanza baada ya kocha kurejea. Amewaambia viongozi kuwa akishirikiana na kina Kelvin Yondani, Yanga itakuwa imara sana nyuma.

Fiston atajaribiwa kwa wiki mbili ambapo endapo uwezo wake utakubalika, atasaini mkataba wa awali na Yanga na kurejea klabuni kwake.

Imeelezwa kuwa atarejea tena nchini kuja kujiunga na mabingwa watetezi hao wa Ligi Kuu Bara wakati wa usajili wa dirisha dogo la usajili likalaofunguliwa Novemba.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA ILIVYONUSURIKA KUSHUKA DARAJA MWAKA 1989

TUJIKUMBUSHE MECHI KALI KATI YA YANGA NA SIMBA NYAMAGANA 1974?

JINSI YANGA ILIVYOIADHIBU SIMBA MWAKA 1994