AZAM FC YAFURAHIA MECHI ZAKE NA YANGA KUPELEKWA CHAMANZI

Mabadiliko ya ratiba mpya ya Ligi Kuu yanaonyesha kuwa mechi zote za Azam FC za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga zitafanyika Uwanja wa Azam Complex.
 
Klabu ya Azam FC imefuraishwa na taarifa za shirikisho la mpira TFF kuruhusu mechi zao dhidi ya  Simba na Yanga kufanyika kwenye uwanja wao wa Chamanzi.

Kwa mara ya kwanza mechi ya Azam na Simba itafanyika katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Jumamosi hii Septemba 9.

" Ni furaha tupu ndani ya viunga vya Azam Complex kwenye makao makuu ya Klabu BIngwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuiruhusu timu hiyo kutumia uwanja huo kwa mara ya kwanza kwenye mechi zake za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga. waliandika hivyo kupitia kwenye mtandao wao wa klabu.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA ILIVYONUSURIKA KUSHUKA DARAJA MWAKA 1989

TUJIKUMBUSHE MECHI KALI KATI YA YANGA NA SIMBA NYAMAGANA 1974?

JINSI YANGA ILIVYOIADHIBU SIMBA MWAKA 1994