TAMBWE"NIMEMISSI KUIFUNGA SIMBA"
Mshambuliaji wa Yanga raia wa Burundi, Amissi Tambwe amesema ana hamu ya kuitungua klabu ya Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii siku ya Jumatano
Akizungumza na gazeti la michezo la Champion, Mrundi huyo amesema kuwa ana hamu kubwa sana ya kuona akizifumania nyavu siku hiyo kwani amemisi kuifunga timu hiyo.
“Namshukuru Mungu hivi sasa nipo fiti na ninaendelea vizuri na maandalizi yangu kuelekea mchezo huo baada ya kupona goti lililokuwa likinisumbua hivi karibuni.
“Ninamshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema na nipo tayari kwa ajili ya mechi ya Jumatano dhidi ya Simba, kwani nimemisi sana kuifunga jambo ambalo linanifanya nijisikie vibaya kila wakati.
“Endapo nitapata nafasi ya kuanza hiyo Jumatano dhidi ya Simba, nitahakikisha napambana vilivyo ili niweze kuzifumania nyavu roho yangu itulie kwani nataka nizidi kuandika rekodi ya kuifunga mara nyingi,” alisema Tambwe.
Comments
Post a Comment