TAMBWE NA CHIRWA KUISUBIRI SIMBA
Lwandamina ameiambia YOUNGA AFRICAN, kuwa analazimika kuwaacha wachezaji hao ili waweze kupona vizuri na atawatumia kuanzia mchezo dhidi ya Ndanda FC, ambao utapigwa Dar es Salaam Septemba 23 na ule dhdi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa Septemba 30.
“Wanakosa fitness ndiyo maana nataka kuwapumzisha ili wafanye mazoezi kwa muda mrefu zaidi lengo ni kuwaanda kwa ajili ya mechi hizo na nyingine ambazo tutakwenda kucheza kanda ya Ziwa kabla ya kupambana na Simba Oktoba 28,”amesema Lwandamina.
Kocha huyo raia wa Zambia amesema maandalizi yao yanakwenda vizuri kuhakikisha wanashinda mechi hizo mbili ambazo wanakwenda kucheza kwenye mikoa ya Njombe na Ruvuma.
Amesema kusudio lao ni kurudi Dar es Salaam na pointi sita ambazo zitawaongezea kasi kushinda mechi nyingine mbili watakazocheza nyumbani kabla ya kuwafuata Kagera Sugar na Stand United Shinyanga.
Wakati Lwandamina akitoa taarifa hizo tayari wachezaji hao walishaanza mazoezi mepesi chini ya daktari wa timu hiyo Edward Bavu, na walipania kuisaidia timu yao baada ya kutokuonekana kwenye kikosi cha Yanga tangu kuanza msimu huu.
Kukosekana kwa nyota hao kutamfanya kocha Lwandamina kuendelea kuwategemea Donald Ngoma na Ibrahim Ajibu kwenye safu ya ushambuliaji ambayo kiasi fulani imeonekana kupoteza umakini kutokana na kupoteza nafasi nyingi mwenye mechi iliyopita dhidi ya Lipuli.

Comments
Post a Comment