FURAHA YANGA YAMPATA KAMUSOKO NA KAMBWILI KIPA WA SERENGETI BOY.
Taarifa iliyotolewa na Yanga kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika ni kwamba Kamusoko ameongeza mkataba huo baada ya kufikia makubaliano ya mambo kadhaa.
Katika kuimarisha lango lao, Yanga pia imefanya usajili wa Kabwili ambaye alikuwa na Serengeti Boys katika michuano ya Vijana Afrika mwaka huu nchini Gabon.
Usajili umeifanya Yanga kukamilisha usajili wa nyota wanne wapya ambapo awali ilimsainisha kipa wa African Lyon, Youthe Rostand, beki Abdallah Shaibu pamoja na mshambuliaji Ibrahim Ajib.

Comments
Post a Comment