Cannavaro aipa Yanga ushindi dhidi ya Kagera Sugar
Cannavaro, ameiambia YOUNGA , wamefanya mazoezi ya kutosha kujiandaa na mechi za kanda ya ziwa na anaamini watashinda kutokana na uimara.
“Nashukuru mambo yetu yote yanakwenda vizuri lengo letu ni ushindi na ninamaani hivyo kulingana na matayarisho yetu,” amesmea Cannavaro.
Cannavaro ambaye hajaichezea Yanga hata mechi moja amesema hamasa ni kubwa kwenye kambi yao.
Nahodha huyo amesema pamoja na ligi kuonekana kuwa mgumu lakini wamejipanga kufanya kama msimu uliopita.
Yanga inashika nafasi ya sita kwenye msimamo ikiwa na pointi 2 ambazo ndiyo wanazo kwasasa baada ya kucheza mechi tano za ligi.
Comments
Post a Comment