AJIBU AANZA KUTIMIZA WAJIBU

 
 
 
 
Pamoja na ushindani mkali lakini mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara Yanga ,wameonja ladha ya ushindi kwa kuifunga Njombe Mji 
 
Mshambiliaji wa zamani wa Simba Ibrahim Ajibu leo ameipa pointi tatu klabu yake mpya ya Yanga baada ya kufunga bao pekee lililoipa timu hiyo pointi tatu walipokuwa wanacheza ugenini dhidi ya Njombe Mji ya Ruvuma.

Bao hilo limeifanya Yanga kufikisha pointi nne sawa na timu ya Simba, lakini mabingwa hao wapo kwenye nafasi ya tano kwenye msimamo huku Simba wakiongoza ligi hiyo kwa tofauti ya mabao.

Ajibu alifunga bao hilo mapema dakika ya 16, akipiga mpira wa adhabu ndogo uliompita kipa wa Njombe Mji David Kisu na mpira kujaa wavuni.

Wenyeji Njombe Mji ndio waliouanza mchezo huo kwa kasi lakini baada ya dakika tano walijikuta wakikaribisha mashambulizi ya Yanga kwenye lango lao na kufungwa bao hilo ambalo lilidumu kwa muda wote wa mchezo.

Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma alipoteza nafasi ya wazi ya kuifungia timu yake bao la pili kufuatia pasi nzuri ya Gadiel Machael lakini shuti lake lilipaa juu ya lango la Njombe Mji.

Mshambuliaji Ditram Nchimbi wa Njombe Mji alikuwa mwiba mkali kwa mabeki wa Yanga kwani muda wote wa mchezo alionekana kuwasumbua lakini miguu yake ilionekana kukosa macho kwani kila alipojaribu kufunga mashuti yake hayakuweza kulenga lango.

Kipa wa Yanga Youth Rostand, muda mwingi alionekana kuwa likizo kutokana na wapinzani wao kutofika mara kwa mara kwenye lango lake na mashambulizi mengi kuelekezwa kwenye lango lao ambapo beki Raban Kambole na Agaton Mapunda walionekana kufanya kazi ya ziada ili kuokoa mashambulizi hayo.

Kipindi cha pili kocha wa Njombe Mji Hassani Banyai, alifanya mabadiliko kwa kumtoa  Awadhi Salum ambaye alionekana kushindwa kuisaidia timu yake kwenye eneo la kiungo.

Mbadiliko hayo yalionekana kuiimarisha Njombe na kuanza kuishmbulia sana Yanga lakini walishindwa kutumia vizuri nafasi walizozipata kwenye mchezo huo.

Kipa wa Yanga Rostand alifanya kazi kubwa na yaziada kwenye mchezo huo kwa kuokoa mashambulizi mengi ya wenyeji wao baada ya wachezaji wake kuchoka huku upepo ukiwa ni moja ya sababu iliyowachangia mipira kushindwa kukaa mbele.

Huo ni ushindi wa kwanza kwa Yanga tangu kuanza kwa msimu huu ambapo katika mchezo wa kwanza uliokuwa wa ufunguzi timu hiyo ikiwa nyumbani uwanja wa Uhuru iliweza kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Lipuli ya Iringa.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA ILIVYONUSURIKA KUSHUKA DARAJA MWAKA 1989

TUJIKUMBUSHE MECHI KALI KATI YA YANGA NA SIMBA NYAMAGANA 1974?

JINSI YANGA ILIVYOIADHIBU SIMBA MWAKA 1994