KAMATI IMENITENDEA HAKI...

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa ameachiwa huru na Kamati ya masaa 72 ambayo ipo chini ya Bodo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara. 
 
Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia anayekipiga kwenye klabu ya Yanga Obrey Chirwa amesema anafurahi kwa kuachiwa huru na Kamati ya Nidhamu na Sheria ya TFF.

Chirwa ameiambia SOKA DUNIANI, Kamati imetenda haki kwani yeye hakuhusika kabisa kwenye tukio lile lakini ni muda wake sasa kujipanga kwa ajili ya kuipigania timu yake kwenye mechi za ligi zinazoendelea.

“Nashukuru kuona nimekutwa sina hatia kwasasa najipanga kwa ajili ya kuipigania timu yangu iweze kufanya vizuri kwenye ligi,”amesema Chirwa.

Kwa pamoja, wakiwa wachezaji wa Yanga, Chirwa, Kaseke na winga mpya wa Difaa Hassan El- Jadida walidaiwa kumsukuma na kumwangusha refa Ludovic Charles katika mechi namba 236 ya Ligi Kuu iliyokutanisha timu hiyo na wenyeji, Mbao FC walioibuka na ushindi wa 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Hata hivyo, baada ya kikao cha jana, wote Kaseke na Chirwa wamekutwa hawana hatia, huku Msuva pekee akitiwa hatiani na kupewa onyo kali.

Wachezaji hao walidaiwa kufanya kitendo hicho katika mechi hiyo dhidi ya Mbao FC iliyofanyika Mei 20, 2017 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijni Mwanza. Uamuzi wa Kamati ya Saa 72 ulizingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu.

Lakini refa, Ludovic Charles naye alipewa onyo kali kwa kutoumudu mchezo kwa mujibu wa Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA ILIVYONUSURIKA KUSHUKA DARAJA MWAKA 1989

TUJIKUMBUSHE MECHI KALI KATI YA YANGA NA SIMBA NYAMAGANA 1974?

JINSI YANGA ILIVYOIADHIBU SIMBA MWAKA 1994