LWANDAMINA AENDA KWAO ZAMBIA
Lwandamina ameiambia Goal, atakuwa huko hadi shuhuli za msiba zitakapo malizika ndipo atarudi Dar es Salaam kuendelea na kazi yake ya kukinoa kikosi cha Yanga.
“Nakwenda nyumbani kwenye msiba wa Baba yangu baada ya kumaliza msiba nitarudi kazi kwa ajili ya kuiongoza Yanga kwenye michuano inayotukabili ya ligi ,”amesema Lwandamina.
Kocha huyo amesema baada ya yeye kuondoka majukumu yote ya timu amemuachia msaidizi wake Shedrack Nsajigwa pamoja akiamini anaweza kuwasimamia vizuri.
Amesema anatambua presha iliyopo baada ya kuanza na sare kwenye mechi yao ya kwanza msimu huu hivyo wanajipanga kuhakikisha wanafanya vizuri na kutwaa kutetea ubingwa wao.
Yanga kwasasa inashika nafasi 10 kwenye msimamo ikiwa na pointi moja baada ya kulazimishwa sare ya kufungana mabao 1-1 na Lipuli ya Iringa.

Comments
Post a Comment