YONDANI AULA TAIFA STARS




Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Salum Mayanga amemrudisha beki Kelvin Yondani kwenye kikosi cha Taifa Stars ambacho kitapambana na Botswana Sap 2 
 
Kocha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Salum Mayanga, ameita kikosi cha wachezi 21, kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Botswana.

Mayanga ameiambia YOUNGA AFRICAN, kikosi hicho kitaingia kambini kesho kujiandaa na mchezo huo ambao ni maandalizi kwa ajili ya kujiandaa na mechi za kufuzu fainali ya Mataifa ya Afrika.

“Timeita kikosi kulingana na kiwango cha mchezaji pamoja na nidhamu yake kwani naamini wachezaji hao wataitikia wito mapema na tutafanya vizuri kwenye mchezo huo,” amesema Mayanga.

Katika kikosi hicho alichokitaja leo Mayanga amemrejesha beki mkongwe wa Yanga, Kevin Yondan

Mayanga amesema kwamba kwa sababu ya majeruhi hajawaita kipa Said Mohammed ‘Ndunda’ na mshambuliaji John Raphael Bocco, wote wa Simba.

Mayanga amesema kwa sababu kama hizo pia hajamuita kipa wa Yanga, Beno Kakolanya kwa ajili ya maandalizi mchezo wa kirafiki dhidi ya Botswana Septemba 2, mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na badala yake amemrejesha Mwadini Ali wa Azam.

Kwa ujumla kikosi kamili cha Stars alichoteua Mayanga kinaundwa na
makipa; Aishi Manula (Simba), Mwadini Ali (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Yanga SC).

Mabeki; Gardiel Michael (Yanga), Boniface Mganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC, Afrika Kusini), Kelvin Yondan (Yanga), Salim Mbonde (Simba) na Erasto Nyoni (Simba).

Viungo; Himid Mao (Azam FC), Hamisi Abdalla (Sony Sugar, Kenya), Muzamil Yassin (Simba), Said Ndemla (Simba), Simon Msuva (Difaa Hassan El- Jadida, Morocco), Shiza Kichuya (Simba), Farid Mussa
(Tenerrife B, Hispania) na Morel Ergenes (FC Famalicao/Ureno).

Washambuliaji; Rafael Daudi (Yanga), Kelvin Sabato (Mtibwa Sugar), Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji) na Elius Maguli (Dhofar FC, Oman).

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA ILIVYONUSURIKA KUSHUKA DARAJA MWAKA 1989

TUJIKUMBUSHE MECHI KALI KATI YA YANGA NA SIMBA NYAMAGANA 1974?

JINSI YANGA ILIVYOIADHIBU SIMBA MWAKA 1994