NATISHA SABABU YA KOCHA WANGU-MSUVA
Msuva ameiambia YOUNGA AFRICAN, kwa muda mfupi alioichezea timu hiyo ameweza kujifunza mengi ikiwemo mbinu za kuwatoroka na mabeki na kufunga mabao kama aliyofunga jana na kuipa ushindi wa mabao 2-0 Tanzania.
“Naweza kusema bado kuna mambo mazuri zaidi yanakuja kutoka kwangu kwani huu ndiyo mwanzo hata ligi haijaanza lakini nimekuwa na mwanzo mzuri ambao mpaka sasa miweza kufunga mabao 9 katika mechi 12 za kirafiki nilizocheza,”amesema Msuva.
Mshambuliaji huyo wa pembeni pia amemshukuru kocha Salum Mayanga kwa kumuita kwenye kikosichake na kumpa nafasi ya kucheza hata kuonyesha kile ambacho alikuja nacho kwa ajili ya kuwazawadia Watanzania.
Amesema mchezo ulikuwa mgumu lakini mazoezi aliyokuwa nayo yamemsaidia na kuweza kucheza vizuri na kuisaidia timu yake kupata ushindi huo ambao anaamini utawasaidia kupanda kwenye viwango vya FIFA.
Aidha mshambuliaji huyo amewapa changamoto wachezaji wa Tanzania kwa kuwataka wazidi kupambana ili kutoka kwenda kucheza nje kwani nafasi zipo endapo watajitambua.
Comments
Post a Comment