KIUNGNO MWENGINE WA RASTA ASINI
Yanga imemsainisha kiungo Raphael Daud kutoka Mbeya City tayari kuitumikia klabu hiyo na leo Ijumaa timu inatarajiwa kutua kambini mjini Morogoro kuungana na wachezaji wenzao kwa maandalizi ya msimu mpya wa mashindano.
Habari kutoka kwa mabosi wa Yanga, ni kwamba Rafael alisainishwa mkataba huo juzi Jumatano, lakini waliamua kufanya siri kwa sababu kuna mambo hawajamalizana na klabu yake ya City.
“Rasta amesaini tayari kuanza kuitumikia Yanga, lakini pia tumemalizana na kiungo Rafael Daud ambaye tulishaanza mazungumzo naye mapema, lakini ikawa bado kusaini kitu kilichokamilika juzi,” kilisema chanzo hicho makini.
Yanga ilikamilisha dili la Papii anayetokea Mbabane Swallows ya Swaziland, baada ya juzi kumfanyia vipimo vya afya siku chache tangu alipotua nchini ili kuja kumalizana na mabosi wa Yanga.
Papii alisaini mkataba huo mchana wa jana na kuifanya Yanga sasa kusaliwa na nafasi moja kwa nyota wa kigeni ambayo inawaniwa na Mnigeria Henry Tony Okoh na Mkameruni Fernando Bongyang

Comments
Post a Comment