Posts

Donald Ngoma kuzikosa mechi za kanda ya ziwa

Image
Ngoma amefanikiwa kufunga magoli 2 katika mechi 5 za Ligi Kuu mpaka sasa.    Kocha wa Yanga,  George Lwandamina atamkosa mshambuliaji wake hatari raia wa Zimbabwe Donald Ngoma, baada ya taarifa ya daktari wa timu hiyo kuthibitisha ukubwa wa tatizo alilokuwa nalo. Lwandamina ameiambia Goal,  kumkosa Ngoma ni lengo kubwa katika safi yake ya ushambuliaji hasa katika mechi ngumu inayowakabili Jumamosi hii dhidi ya Kagera  Sugar. "Ngoma ni mchezaji muhimu kwenye kikosi changu kumkosa ni pengo kubwa ingawa nafuahia kurejea kwa Amissi Tambwe ambaye Naye alikuwa majeruhi tangu kuanzia kwa msimu huu" amesema Lwandamina. Kocha huyo raia wa Zambia amesema taarifa ya daktari Edward Bavu,  imemhuzunisha lakini hawezi kupingana na ukweli uliopo mbele yake. Lwandamina mategemeo yake kwasasa kwenye safi ya ushambuliajo yatabaki kwa Ibrahim Ajibu na Tambwe huku pia akiamini wachezaji Obrey Chirwa na Emmanuel Martini watafanya...

Timu za Ligi Kuu Bara zenye wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram

Image
Yanga: Wanashika nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram, in wafuasi elfu 82  Azam: Waoka Mikate hao wa Dar es salaam, wanajumla ya wafuasi 108,000 kwenye akaunti yao ya Instagram, ana shika nafasi ya pili nyuma ya klabu ya Simba.  Simba: Ndiyo klabu yenye wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram hapa nchini, ina jumla ya wafuasi ya zaidi ya 196,000  Mbeya City: Anazidiwa wafuasi na klabu za Dar es salaam pekee, ana kamata nafasi ya nne baada ya kuwa na wafuasi 64 katika akaunti yake ya Instagram.  Mtibwa Sugar: ana jumla ya wafuasi 38 katika akaunti yake, ana kamata nafasi ya tano kwa klabu zenye wafuasi wengi Instagram.

Cannavaro aipa Yanga ushindi dhidi ya Kagera Sugar

Image
Mabingwa watetezi Yanga Oktoba 14 watakuwa ugenini uwanja wa Kaitaba kucheza na Kagera Sugar na nahodha wake Cannavaro ameahidi ushindi    Nahodha mkuu wa klabu ya Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro, amesema wamejipanga kucheza kwa bidii ili kuweza kushinda mechi yao dhidi ya Kagera Sugar. Cannavaro, ameiambia YOUNGA , wamefanya mazoezi ya kutosha kujiandaa na mechi za kanda ya ziwa na anaamini watashinda kutokana na uimara. “Nashukuru mambo yetu yote yanakwenda vizuri lengo letu ni ushindi na ninamaani hivyo kulingana na matayarisho yetu,” amesmea Cannavaro. Cannavaro ambaye hajaichezea Yanga hata mechi moja amesema hamasa ni kubwa kwenye kambi yao. Nahodha huyo amesema pamoja na ligi kuonekana kuwa mgumu lakini  wamejipanga kufanya kama msimu uliopita. Yanga inashika nafasi ya sita kwenye msimamo ikiwa na pointi 2 ambazo ndiyo wanazo kwasasa baada ya kucheza mechi tano za ligi.

Yanga watamba kurudi na pointi 6 Kanda ya Ziwa

Image
Uongozi wa Yanga umeahidi kurudi na pointi sita katika mechi zao mbili watakazokwenda kucheza kwenye mikoa ya Kagera na Mwanza kuanzia Jumamosi ijayo Mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga wanatarajia kuoandoka Dar es Salaam, Alhamisi kuelekea mkoani Kagera, kwa ajili ya pambano lao la Jumamosi dhidi ya Kagera Sugar. Msemaji wa Yanga Dismas Ten, ameiambia Goal , kikosi chao kinatarajia kuondoka na nyota wake wote kuelekea Kagera na Mwanza, kwa ajili ya mechi hizo ambazo wamepanga kushinda na kurudi na pointi zote sita. “Tunakwenda kucheza mechi mbili dhidi ya Kagera Sugar na Mbao na zote ni mechi ngumu na ukweli tumepania kushinda ndiyo maana tunakwenda mapema tukiwa na kikosi chetu kamili,” amesema Ten. Msemaji huyo amesema wachezaji wao wote wapo sawa na hakuna aliyekuwa majeruhi jambo ambalo linawapa matumaini ya kutimiza kile ambacho wamekikusudia kukifanya kwenye mechi hizo. Msemaji huyo aliyewahi kufanya kazi na klabu ya Mbeya...

LIGI KUU BARA...WACHEZAJI MAHIRI KUPIGA MIPIRA YA ADHABU NDOGO

Image
                       Ibrahim Ajibu |  Amekuwa akifunga magoli ya mipira ya adhabu mara kwa mara tangu akiwa Simba, msimu huu tayari amesha fanya hivyo dhidi ya Njombe Mji                   Thaban Kamusoko |  Tangu ajiunge na Yanga misimu mitatu nyuma amekuwa ndiye mpigaji maalumu wa mipira ya adhabu, Hajawahi kufanya kosa                 Shiza Kichuya |  Amejizolea umaarufu katika kipengele cha kupiga mipira ya adhabu maarufu kama "Kichuya Kona".                   Emmanuel Okwi |  Ni mara ya tatu anarudi kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara, awamu moja Yanga na hii ni ya tatu kwa Simba, msimu huu bado hajaonyesha cheche zake, lakini anak...

NATAKA KUFUNDISHA YANGA

Image
Nahodha wa Yanga Nadiri Haroub amesema hachukii maamuzi ya kocha wake George Lwandamina kumuweka benchi na zaidi anajifunza ili kuja kuwa kocha    Nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema atakapostaafu kucheza soka anataka kusomea ukocha ili kuja kuchukua mikoba ya kocha wake wa sasa George Lwandamina. Cannavaro licha ya kuwa na cheo hicho lakini amekuwa hapati nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kutokana na umri wake kumtupa mkono. “Hata kama sichezi lakini nafurahi kuwa benchi kwasababu najifunza mambo mengi kutoka kwa makocha waliopo na lengo langu baada ya kustaafu kucheza nataka kuja kuifundisha Yanga siku zijazo,” amesema Cannavaro. Nahodha huyo ameiambia YOUNGA AFRICAN ,  hakuna kinachoshindikana katika hilo kwani kwakipindi cha misimu 11, alichoitumikia Yanga ameweza kujifundisha mambo mengi kutoka kwa makocha mbalimbali ambao wamepitia timu hiyo. Mkongwe huyo amesema mipango yake baada ya kustaafu kucheza soka ni kwenda...

AJIBU AANZA KUTIMIZA WAJIBU

Image
        Pamoja na ushindani mkali lakini mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara Yanga ,wameonja ladha ya ushindi kwa kuifunga Njombe Mji    Mshambiliaji wa zamani wa Simba Ibrahim Ajibu leo ameipa pointi tatu klabu yake mpya ya Yanga baada ya kufunga bao pekee lililoipa timu hiyo pointi tatu walipokuwa wanacheza ugenini dhidi ya Njombe Mji ya Ruvuma. Bao hilo limeifanya Yanga kufikisha pointi nne sawa na timu ya Simba, lakini mabingwa hao wapo kwenye nafasi ya tano kwenye msimamo huku Simba wakiongoza ligi hiyo kwa tofauti ya mabao. Ajibu alifunga bao hilo mapema dakika ya 16, akipiga mpira wa adhabu ndogo uliompita kipa wa Njombe Mji David Kisu na mpira kujaa wavuni. Wenyeji Njombe Mji ndio waliouanza mchezo huo kwa kasi lakini baada ya dakika tano walijikuta wakikaribisha mashambulizi ya Yanga kwenye lango lao na kufungwa bao hilo ambalo lilidumu kwa muda wote wa mchezo. Mshambuliaji wa Yanga Donald ...