MRITHI SAHIHI WA CHUJI APATIKANA YANGA
Hakuna shaka juu ya hilo.Athuman Idd Chuji alikuwa mchezaji mahiri enzi zake.Akicheza kama kiungo mkabaji,alionyesha uwezo wake na kuwa tishio kwa timu pinzania,Si hapa nchini tu bali pia aliogopwa na kusifiwa hadi nje ya nchi,
Lakini tangu alipoondoka yanga,Timu hiyo imeshindwa kumpata mrithi wa kuchukua nafasi yake.Wamejaribiwa wengi lakini hakuna aliyeonyesha au kuukaribia uwezo wa Chuji.
Anaitwa Papi Kabamba Tshishimbi.Alikuwa mchezaji wa Mbabane Swallows na alikuja Tanzania kwa mara ya kwanza na timu yake kuvaana na Azam kwenye mchezo wa kwanza wa mtoano wa Kombe la shirikisho.Kiwango chake kilimvutia kocha George Lwandamina na akaamua kumuwekea mashushushu wa kujua ni nani hasa mchezaji huyu.Lwandamina mwenyewe alifika hadi Swaziland kumshuhudia mchezaji huyu katika moja ya mechi alizocheza akiwa na Mbabane Swallows...akaridhika nae.
Ni jana tu ,jamaa huyu akatia timu Tanzania kimya kimya na kuanza mazungumzo na uongozi wa Yanga,Mda si mrefu atatambulishwa na kwa aina ya washambuliaji walioko yanga.tutegemee mauaji maanake jamaa ni mkali hasa,,,,Ana uwezo mkubwa hasa wa kupiga pasi ndefu....Hapotezi mpira kizembe na pasi zake nyingi mara nyingi zina macho,,,,zinaona!!!!Zote hizo ni sifa alizokuwa nazo Chuji,Kwa stahili hii,Chuji kapata mrithi wake hasa pale Jangwani


Comments
Post a Comment