SARE KITU GANI? SUBIRI MZIKI WETU
Kocha
wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara George Lwandamina
amesema sare waliyoipata jana dhidi ya Lipuli FC haijawavurugia mipango
ya kutetea ubingwa wao.
Lwandamina ameiambia SOKA DUNIANI timu yake ilicheza vizuri lakini wapinzani wao waliziba njia walizopanga kuzitumia ndiyo mana wakapata sare.
"Tulicheza vizuri wachezaji walijituma lakini tukashindwa kutumia nafasi tulizozipata lakini hilo halitutoi kwenye mbio za ubingwa kwasababu ndiyo mchezo wa kwanza bado tuna michezo mingi," amesema.
Mzambia huyo amesema kuwa wapinzani wao waliingia kwa kuwakamia na kuwachezea rafu baadhi ya wachezaji wake kitu ambacho kilivuruga mipango yao.
Amesema wanetambua mapungufu yao na wanakwenda kuyafanyia kazi akiamini kwamba mchezo unaofuata dhidi ya Njombe Mji watarekebisha na kupata matokeo.
Yanga ilianza vibaya harakati za kutetea ubingwa wake msimu huu baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Comments
Post a Comment