NATAKA KUFUNDISHA YANGA
Cannavaro licha ya kuwa na cheo hicho lakini amekuwa hapati nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kutokana na umri wake kumtupa mkono.
“Hata kama sichezi lakini nafurahi kuwa benchi kwasababu najifunza mambo mengi kutoka kwa makocha waliopo na lengo langu baada ya kustaafu kucheza nataka kuja kuifundisha Yanga siku zijazo,” amesema Cannavaro.
Nahodha huyo ameiambia YOUNGA AFRICAN, hakuna kinachoshindikana katika hilo kwani kwakipindi cha misimu 11, alichoitumikia Yanga ameweza kujifundisha mambo mengi kutoka kwa makocha mbalimbali ambao wamepitia timu hiyo.
Mkongwe huyo amesema mipango yake baada ya kustaafu kucheza soka ni kwenda kusomea ukocha ili kuongeza elimu ambayo itamfanya kuwa na vigezo vya kuweza kufundisha timu za Ligi Kuu hasa Yanga.
Cannavaro alijiunga na Yanga mwaka 2007, akitokea Tembo ya Zanzibar akiwa na wenzake watatu ambao ni kipa Mbarouk Selemani, Mohamed Mkweche na Thomas Morice.
Comments
Post a Comment