KAMUSOKO SI WA KAWAIDA;;;;HAJI MANARA
Thabani Kamusoko alijiunga na Yanga misimu miwili nyuma akitokea klabu ya FC Platnumz ya nchini Zimbabwe.
Katika misimu mitatu Jangwani, Kamusoko amefanikiwa kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu Bara, moja la FA na Ngao ya Jamii, kadhalika na kuiwezesha Yanga kucheza hatua ya makundi, kombe la Shirikisho Afrika misimu miwili nyuma chini ya mwalimu, Hans Van Pluijm.
Akitumia akaunti yake ya Instagram, Haji Manara amesema kiungo huyo si wakucheza nchini hapa kutokana na uwezo wake mkubwa
"Huwa sifichi mahaba yangu kwa mchezaji anayenivutia uwanjani, hata kama anachezea Klabu nisiyoishabikia, Scara kamusoko hapewi heshma anayostahili nchi hii, ni level ya kucheza Europe"
Comments
Post a Comment