NGOMA APANIA KUIFUNGA SIMBA KESHO

Mshambuliaji wakimataifa wa Yanga Donald Ngoma amesema atahakikisha anaifungia bao timu yake kesho wakati ikipambana na Simba uwanja wa Taifa Dar 
Mshambuliaji wa Yanga raia wa Zimbabwe Donald Ngoma, amesema yupo fiti kwa ajili ya kuwaangamiza Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utapigwa kesho uwanja wa Taifa.
Ngoma ameiambia YOUNGA AFRICAN, haoni ugumu wowote kuelekea mchezo huo na hiyo ni kutokana na kupona majeruhi yaliyomsumbua kwa muda mrefu na ubora wa kikosi chao ulivyo.

“Bado sijaona beki wa Simba ambaye anaweza kunizuia kwanza nina hasira nao sana baada ya kukosa mechi mbili za msimu uliopita imeniuma sana walivyotufunga na nisingependa matokeo yale yajirudie tena,”amesema Ngoma.

Mshambuliaji huyo aliyeongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga, amesema anataka kurudisha heshima Yanga kama ilivyokuwa wakati wa nyuma ambapo waliweza kutamba kwa kuzifunga timu zote kubwa nchini.

Amesema ili kuthibitisha kuwa wao ni timu kubwa nilazima waifunge Simba kesho ili kujiweka katika mazingira mazuri hata ya kutetea taji lao la ligi ya Vodacom Tanzania Bara.

Ngoma ameifunga Simba mara moja tangu alipotua nchini misimu miwili iliyopita akitokea FC Platinum ya kwao Zimbabwe sambamba na kiungo mkongwe Thabani Scara Kamusoko.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA ILIVYONUSURIKA KUSHUKA DARAJA MWAKA 1989

TUJIKUMBUSHE MECHI KALI KATI YA YANGA NA SIMBA NYAMAGANA 1974?

JINSI YANGA ILIVYOIADHIBU SIMBA MWAKA 1994