Posts

Showing posts from October, 2017

Donald Ngoma kuzikosa mechi za kanda ya ziwa

Image
Ngoma amefanikiwa kufunga magoli 2 katika mechi 5 za Ligi Kuu mpaka sasa.    Kocha wa Yanga,  George Lwandamina atamkosa mshambuliaji wake hatari raia wa Zimbabwe Donald Ngoma, baada ya taarifa ya daktari wa timu hiyo kuthibitisha ukubwa wa tatizo alilokuwa nalo. Lwandamina ameiambia Goal,  kumkosa Ngoma ni lengo kubwa katika safi yake ya ushambuliaji hasa katika mechi ngumu inayowakabili Jumamosi hii dhidi ya Kagera  Sugar. "Ngoma ni mchezaji muhimu kwenye kikosi changu kumkosa ni pengo kubwa ingawa nafuahia kurejea kwa Amissi Tambwe ambaye Naye alikuwa majeruhi tangu kuanzia kwa msimu huu" amesema Lwandamina. Kocha huyo raia wa Zambia amesema taarifa ya daktari Edward Bavu,  imemhuzunisha lakini hawezi kupingana na ukweli uliopo mbele yake. Lwandamina mategemeo yake kwasasa kwenye safi ya ushambuliajo yatabaki kwa Ibrahim Ajibu na Tambwe huku pia akiamini wachezaji Obrey Chirwa na Emmanuel Martini watafanya...

Timu za Ligi Kuu Bara zenye wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram

Image
Yanga: Wanashika nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram, in wafuasi elfu 82  Azam: Waoka Mikate hao wa Dar es salaam, wanajumla ya wafuasi 108,000 kwenye akaunti yao ya Instagram, ana shika nafasi ya pili nyuma ya klabu ya Simba.  Simba: Ndiyo klabu yenye wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram hapa nchini, ina jumla ya wafuasi ya zaidi ya 196,000  Mbeya City: Anazidiwa wafuasi na klabu za Dar es salaam pekee, ana kamata nafasi ya nne baada ya kuwa na wafuasi 64 katika akaunti yake ya Instagram.  Mtibwa Sugar: ana jumla ya wafuasi 38 katika akaunti yake, ana kamata nafasi ya tano kwa klabu zenye wafuasi wengi Instagram.

Cannavaro aipa Yanga ushindi dhidi ya Kagera Sugar

Image
Mabingwa watetezi Yanga Oktoba 14 watakuwa ugenini uwanja wa Kaitaba kucheza na Kagera Sugar na nahodha wake Cannavaro ameahidi ushindi    Nahodha mkuu wa klabu ya Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro, amesema wamejipanga kucheza kwa bidii ili kuweza kushinda mechi yao dhidi ya Kagera Sugar. Cannavaro, ameiambia YOUNGA , wamefanya mazoezi ya kutosha kujiandaa na mechi za kanda ya ziwa na anaamini watashinda kutokana na uimara. “Nashukuru mambo yetu yote yanakwenda vizuri lengo letu ni ushindi na ninamaani hivyo kulingana na matayarisho yetu,” amesmea Cannavaro. Cannavaro ambaye hajaichezea Yanga hata mechi moja amesema hamasa ni kubwa kwenye kambi yao. Nahodha huyo amesema pamoja na ligi kuonekana kuwa mgumu lakini  wamejipanga kufanya kama msimu uliopita. Yanga inashika nafasi ya sita kwenye msimamo ikiwa na pointi 2 ambazo ndiyo wanazo kwasasa baada ya kucheza mechi tano za ligi.

Yanga watamba kurudi na pointi 6 Kanda ya Ziwa

Image
Uongozi wa Yanga umeahidi kurudi na pointi sita katika mechi zao mbili watakazokwenda kucheza kwenye mikoa ya Kagera na Mwanza kuanzia Jumamosi ijayo Mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga wanatarajia kuoandoka Dar es Salaam, Alhamisi kuelekea mkoani Kagera, kwa ajili ya pambano lao la Jumamosi dhidi ya Kagera Sugar. Msemaji wa Yanga Dismas Ten, ameiambia Goal , kikosi chao kinatarajia kuondoka na nyota wake wote kuelekea Kagera na Mwanza, kwa ajili ya mechi hizo ambazo wamepanga kushinda na kurudi na pointi zote sita. “Tunakwenda kucheza mechi mbili dhidi ya Kagera Sugar na Mbao na zote ni mechi ngumu na ukweli tumepania kushinda ndiyo maana tunakwenda mapema tukiwa na kikosi chetu kamili,” amesema Ten. Msemaji huyo amesema wachezaji wao wote wapo sawa na hakuna aliyekuwa majeruhi jambo ambalo linawapa matumaini ya kutimiza kile ambacho wamekikusudia kukifanya kwenye mechi hizo. Msemaji huyo aliyewahi kufanya kazi na klabu ya Mbeya...