Donald Ngoma kuzikosa mechi za kanda ya ziwa

Ngoma amefanikiwa kufunga magoli 2 katika mechi 5 za Ligi Kuu mpaka sasa. 
 
Kocha wa Yanga,  George Lwandamina atamkosa mshambuliaji wake hatari raia wa Zimbabwe Donald Ngoma, baada ya taarifa ya daktari wa timu hiyo kuthibitisha ukubwa wa tatizo alilokuwa nalo.

Lwandamina ameiambia Goal,  kumkosa Ngoma ni lengo kubwa katika safi yake ya ushambuliaji hasa katika mechi ngumu inayowakabili Jumamosi hii dhidi ya Kagera  Sugar.

"Ngoma ni mchezaji muhimu kwenye kikosi changu kumkosa ni pengo kubwa ingawa nafuahia kurejea kwa Amissi Tambwe ambaye Naye alikuwa majeruhi tangu kuanzia kwa msimu huu" amesema Lwandamina.

Kocha huyo raia wa Zambia amesema taarifa ya daktari Edward Bavu,  imemhuzunisha lakini hawezi kupingana na ukweli uliopo mbele yake.

Lwandamina mategemeo yake kwasasa kwenye safi ya ushambuliajo yatabaki kwa Ibrahim Ajibu na Tambwe huku pia akiamini wachezaji Obrey Chirwa na Emmanuel Martini watafanya vizuri kwenye mechi hizo mbili watakazocheza Kanda ya ziwa.

Ngoma aliumia misuli ya paja kwenye mchezo uliopita wa Logo kuu ya Tanzania bara,  dhidi ya Mtbwa Sugar Jumamosi iliyopita

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA ILIVYONUSURIKA KUSHUKA DARAJA MWAKA 1989

TUJIKUMBUSHE MECHI KALI KATI YA YANGA NA SIMBA NYAMAGANA 1974?

JINSI YANGA ILIVYOIADHIBU SIMBA MWAKA 1994