Yanga watamba kurudi na pointi 6 Kanda ya Ziwa
Msemaji wa Yanga Dismas Ten, ameiambia Goal, kikosi chao kinatarajia kuondoka na nyota wake wote kuelekea Kagera na Mwanza, kwa ajili ya mechi hizo ambazo wamepanga kushinda na kurudi na pointi zote sita.
“Tunakwenda kucheza mechi mbili dhidi ya Kagera Sugar na Mbao na zote ni mechi ngumu na ukweli tumepania kushinda ndiyo maana tunakwenda mapema tukiwa na kikosi chetu kamili,” amesema Ten.
Msemaji huyo amesema wachezaji wao wote wapo sawa na hakuna aliyekuwa majeruhi jambo ambalo linawapa matumaini ya kutimiza kile ambacho wamekikusudia kukifanya kwenye mechi hizo.
Msemaji huyo aliyewahi kufanya kazi na klabu ya Mbeya City, amesema baada ya mechi yao ya juzi dhidi ya KMC ya Daraja la kwanza na kushindwa kufungana wanatarajia kuanza mazoezi kesho Jumanne na Jumatano kabla ya Alhamisi kuanzasafari ya Kagera.
Yanga inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, wakiwa na pointi 9, katika mechi tano walizocheza msimu huu.
Comments
Post a Comment