Posts

Showing posts from August, 2017

KUNA PRESHA KUBWA KUCHEZA YANGA KULIKO AZAM

Image
Hivi karibuni Gadiel, alijiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Azam ambako alianzia maisha ya soka la ushindani.    BEKI mpya wa Yanga Gadiel Michael, amesema kuna tofauti kubwa kucheza Yanga na klabu nyingine ndogo ambazo hazina presha kama ilivyokuwa Azam FC. Gadiel, amesema maisha ya Yanga ni mazuri lakini kitu kikubwa kinacho mzingua ni presha ya mashabiki ambao kila mechi wanahitaji mchezaji acheze vizuri na timu ipate ushindi. “Kiukweli nimepata mapokezi mazuri kwa wachezaji na hata benchi la ufundi ispokuwa presha ni kubwa kuliko umri wangu tofauti na ilivyokuwa Azam, ingawa nashukuru nifurahi kuona watu wanaikubali kazi yangu,”amesema Gadiel. Beki huyo amesema kitu cha msingi kwake ni kuendelea kucheza kwa kujituma ili kubaki kwenye kikosi cha kwanza vinginevyo anaweza kusota benchi kwani hata msaidizi wake Hajji Mwinyi ni mchezaji mzuri na anaukubali uwezo aliokuwa nao. Amesema atajitahidi kupambana bila uoga ili kuwa...

LWANDAMINA AENDA KWAO ZAMBIA

Image
Kocha wa Yanga George Lwandamina amerudi kwao Zambia leo baada ya kufiwa na mzazi wake wa kiume na atarudi nchini baada ya msiba kwisha    Kocha wa klabu ya Yanga, George Lwandamina ameondoka Dar es Salaam kurudi kwao Zambia, kuhudhiria mazishi ya baba yake mzazi, aliyefariki dunia jana baada ya kusumbuliwa na maradhi ya Kiharusi. Lwandamina ameiambia Goal, atakuwa huko hadi shuhuli za msiba zitakapo malizika ndipo atarudi Dar es Salaam kuendelea na kazi yake ya kukinoa kikosi cha Yanga.  “Nakwenda nyumbani kwenye msiba wa Baba yangu baada ya kumaliza msiba nitarudi kazi kwa ajili ya kuiongoza Yanga kwenye michuano inayotukabili ya ligi ,”amesema Lwandamina. Kocha huyo amesema baada ya yeye kuondoka majukumu yote ya timu amemuachia msaidizi wake Shedrack Nsajigwa pamoja akiamini anaweza kuwasimamia vizuri. Amesema anatambua presha iliyopo baada ya kuanza na sare kwenye mechi yao ya kwanza msimu huu hivyo wanajipanga kuhakikisha wanafanya...

YANGA BINGWA MSIMU HUU ANENA MSUVA

Image
Simon Msuva ana amini kuwa klabu ya Yanga inayo nafasi ya kutetea ubingwa kwa mara ya nne mfululizo    Klabu ya Yanga itakuwa mabingwa wa Ligi Kuu kwa mara nyingine tena kutokana wachezaji wengi kukaa kwa muda mrefu pamoja,  kadhalika na aina ya usajili bora walioufanya msimu huu kwa mujibu wa winga wazamani wa Yanga, Simon Msuva. Msuva amejiunga na klabu ya Difaa el Jadida ya nchini Morocco, kwa dau linalokadiliwa dola 160,000 lilitumika kumg'oa Yanga. “Nimefuatilia mechi za mwanzo za ligi ya Tanzania na nimesikia Simba wameanza kwa kushinda 7-0, wakati timu yangu ya zamani ya Yanga ikitoka sare, watu wengi wanasema Simba itakuwa bingwa, lakini binafsi naona Yanga ndiyo yenye nafasi ya kufanya hivyo tena.alisema hivyo wakati akihojiwa na mtandao wa Salehe Jembe. “Nasema hivyo kwa sababu ukiangalia kweli zote zimefanya usajili wa maana, lakini Yanga ina wachezaji wengi waliokaa pamoja na kuzoeana tofauti na Simba yenye sura nyingi mpya. ...

KAMUSOKO SI WA KAWAIDA;;;;HAJI MANARA

Image
Kwa mujibu wa Haji Manara ana amini kwa uwezo mkubwa alionao Thabani Kamusoko si wakucheza hapa    Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amemvulia kofia kiungo wa klabu ya Yanga Mzimbabwe, Thabani Kamusoko kutokana na umahiri wake mkubwa wa kusukuma kabumbu. Thabani Kamusoko alijiunga na Yanga misimu miwili nyuma akitokea klabu ya FC Platnumz ya nchini Zimbabwe. Katika misimu mitatu Jangwani, Kamusoko amefanikiwa kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu Bara, moja la FA na Ngao ya Jamii, kadhalika na kuiwezesha Yanga kucheza hatua ya makundi, kombe la Shirikisho Afrika misimu miwili nyuma chini ya mwalimu, Hans Van Pluijm. Akitumia akaunti yake ya Instagram, Haji Manara amesema kiungo huyo si wakucheza nchini hapa kutokana na uwezo wake mkubwa "Huwa sifichi mahaba yangu kwa mchezaji anayenivutia uwanjani, hata kama anachezea Klabu nisiyoishabikia, Scara kamusoko hapewi heshma anayostahili nchi hii, ni level ya kucheza Europe "

SARE KITU GANI? SUBIRI MZIKI WETU

Image
Kocha wa Yanga amesisitiza kuwa Yanga bado ipo imara na malengo hayajavurugika ingawa Lipuli walikamia mchezo  Kocha wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara George Lwandamina amesema sare waliyoipata jana dhidi ya Lipuli FC haijawavurugia mipango ya kutetea ubingwa wao. Lwandamina ameiambia SOKA DUNIANI timu yake ilicheza vizuri lakini wapinzani wao waliziba njia walizopanga kuzitumia ndiyo mana wakapata sare. "Tulicheza vizuri wachezaji walijituma lakini tukashindwa kutumia nafasi tulizozipata lakini hilo halitutoi kwenye mbio za ubingwa kwasababu ndiyo mchezo wa kwanza bado tuna michezo mingi," amesema. Mzambia huyo amesema kuwa wapinzani wao waliingia kwa kuwakamia na kuwachezea rafu baadhi ya wachezaji wake kitu ambacho kilivuruga mipango yao. Amesema wanetambua mapungufu yao na wanakwenda kuyafanyia kazi akiamini kwamba mchezo unaofuata dhidi ya Njombe Mji watarekebisha na kupata matokeo. Yanga ilianza vibaya harakati za kutetea ubingwa...

YONDANI AULA TAIFA STARS

Image
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Salum Mayanga amemrudisha beki Kelvin Yondani kwenye kikosi cha Taifa Stars ambacho kitapambana na Botswana Sap 2    Kocha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Salum Mayanga, ameita kikosi cha wachezi 21, kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Botswana. Mayanga ameiambia YOUNGA AFRICAN , kikosi hicho kitaingia kambini kesho kujiandaa na mchezo huo ambao ni maandalizi kwa ajili ya kujiandaa na mechi za kufuzu fainali ya Mataifa ya Afrika. “Timeita kikosi kulingana na kiwango cha mchezaji pamoja na nidhamu yake kwani naamini wachezaji hao wataitikia wito mapema na tutafanya vizuri kwenye mchezo huo,” amesema Mayanga. Katika kikosi hicho alichokitaja leo Mayanga amemrejesha beki mkongwe wa Yanga, Kevin Yondan Mayanga amesema kwamba kwa sababu ya majeruhi hajawaita kipa Said Mohammed ‘Ndunda’ na mshambuliaji John Raphael Bocco, wote wa Simba. Mayanga amesema kwa sababu kama hizo p...

LIPULI LAZIMA IZIKWE

Image
Uzoefu wa Yanga unaweza kuupa mwanzo mzuri na kuweka matumaini ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, msimu huu    Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania bara Yanga LEO wanashuka uwanjani kuwakabili Lipuli FC,  ya Iringa katika pambano ambalo limepangwa kupigwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga itawakosa nyota wake Obrey Chirwa na Pius Buswita kutokana na kesi tofauti ambapo Buswita amesimamishwa mwaka mmoja baada ya kubainika kusaini mara mbili Simba na Yanga. Chirwa licha ya kuwa ni majeruhi lakini pia, alisimamishwa na Kamati ya usimamizi ya uendeshaji Bodi ya ligi ile ya masaa 72 ya msimu uliopita baada ya kumpiga mwamuzi Ludovic Charles katika mchezo wa kumaliza msimu dhidi ya Mbao FC hivyo, anasubiri suala lake kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Yanga imekuwa haitabiriki katika mechi zake za mwanzo kuna wakati huanza vibaya na wakati mwingine hu...

NIYONZIMA NA AJIBU...NANI ATASHINDA?

Pambano lililosubiriwa kwa siku nyingi limefika, ni Simba dhidi ya Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii, Niyonzima na Ajibu wakikabili timu zao za kale    Miamba ya soka Tanzania Yanga na Simba inakutana kesho Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa Ngao ya Jamii ambao unaashiria kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom. Presha imekuwa kubwa kwa pande zote mbili, huku Simba wakiwa na matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo kutokana na usajili ambao wameufanya msimu huu kwa kusajili nyota wenye majina makubwa. Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa ni Februari mwaka huu, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, kwahiyo usajili walioufanya msimu huu pamoja na ushindi walioupata mwisho kumewajengea imani mashabiki wa Simba wakiamini rekodi hiyo itaendelea tena kesho. Kuelekea mchezo huo Yanga wameendelea kujifua kwa kutumia nyota waliosajili kipindi hiki cha usajili ingawa mashabiki wao wameonyesha hofu kutokana na ...

NGOMA APANIA KUIFUNGA SIMBA KESHO

Image
Mshambuliaji wakimataifa wa Yanga Donald Ngoma amesema atahakikisha anaifungia bao timu yake kesho wakati ikipambana na Simba uwanja wa Taifa Dar  Mshambuliaji wa Yanga raia wa Zimbabwe Donald Ngoma, amesema yupo fiti kwa ajili ya kuwaangamiza Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utapigwa kesho uwanja wa Taifa. Ngoma ameiambia YOUNGA AFRICAN , haoni ugumu wowote kuelekea mchezo huo na hiyo ni kutokana na kupona majeruhi yaliyomsumbua kwa muda mrefu na ubora wa kikosi chao ulivyo. “Bado sijaona beki wa Simba ambaye anaweza kunizuia kwanza nina hasira nao sana baada ya kukosa mechi mbili za msimu uliopita imeniuma sana walivyotufunga na nisingependa matokeo yale yajirudie tena,”amesema Ngoma. Mshambuliaji huyo aliyeongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga, amesema anataka kurudisha heshima Yanga kama ilivyokuwa wakati wa nyuma ambapo waliweza kutamba kwa kuzifunga timu zote kubwa nchini. Amesema ili kuthibitisha kuwa wao ni timu kubw...

WACHEZAJI WA KUCHUNGWA SIMBA VS YANGA

Image
Young African inakuletea wachezaji wa kuchungwa kuelekea mchezo wa Yanga na Simba Simba  na Yanga zitashuka dimbani siku ya Jumatano, Agosti 23 uwanja wa Taifa Dar es salaam kwa ajili ya mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii Ukiachana na historia ya pambano hilo, pia ukubwa wa mtanange huo unatokana na nyota wapya waliopo kwenye klabu zote mbili Timu zote mbili zinatarajiwa kuwakosa nyota wake muhimu wa kikosi cha kwanza kutokana na majeraha wanayouguza, Kakolanya, Mwashiuya na Chirwa kwa upande wa Yanga wanatarajiwa kukosekana huku Bocco, Kapombe, Mohammed Hussein kwa upande wa Simba wakiwa na asilimia kubwa ya kuukosa mchezo huo. YOUNG AFRICAN  inakuletea wachezaji wa kuchungwa kuelekea mchezo wa Yanga na Simba Amissi Tambwe - Yanga Amekuwa na rekodi nzuri ya kuifunga Simba tangu ajiunge na Yanga misimu 3 nyuma, Mrundi huyo anaitaji ulinzi mkubwa kumzuia hasa kwa mipira ya hewani, kama kona na krosi Shiza Kichuya - Simba Ni mwi...

TAMBWE"NIMEMISSI KUIFUNGA SIMBA"

Image
Tambwe amefanikiwa kuifunga Simba magoli matatu kwenye mechi tano Mshambuliaji wa Yanga raia wa Burundi, Amissi Tambwe amesema ana hamu ya kuitungua klabu ya Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii siku ya Jumatano Akizungumza na gazeti la michezo la Champion, Mrundi huyo amesema kuwa ana hamu kubwa sana ya kuona akizifumania nyavu siku hiyo kwani amemisi kuifunga timu hiyo. “Namshukuru Mungu hivi sasa nipo fiti na ninaendelea vizuri na maandalizi yangu kuelekea mchezo huo baada ya kupona goti lililokuwa likinisumbua hivi karibuni. “Ninamshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema na nipo tayari kwa ajili ya mechi ya Jumatano dhidi ya Simba, kwani nimemisi sana kuifunga jambo ambalo linanifanya nijisikie vibaya kila wakati. “Endapo nitapata nafasi ya kuanza hiyo Jumatano dhidi ya Simba, nitahakikisha napambana vilivyo ili niweze kuzifumania nyavu roho yangu itulie kwani nataka nizidi kuandika rekodi ya kuifunga mara nyingi,” alisema Tambwe.

CHIRWA KUIKOSA SIMBA NGAO YA JAMII

Image
Shirikisho la soka Tanzania TFF, limemuengua Obrey Chirwa, kwenye kikosi cha Yanga kitakacho ikabili Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii  Yanga itamkosa mshambuliaji wake wa pembeni katika pambano la Ngao ya Jamii Jumatano Mzambia Obrey Chirwa kutokana na adhabu ya kadi ya kumwangusha refa katika mchezo wa ligi ya Vodacom dhidi ya Mbao FC msimu uliopita. Msemaji wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, Alfred Lucas ameiambia Soka Duniani, adhabu ya Chirwa inatumika pande zote mbili kwenye mechi ya ligi pamoja na michuano ya FA. “Tunawatahadharisha Yanga wasije kumtumia Chirwa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii Jumotano dhidi ya Simba kwasababu anatumikia adhabu aliyopata kwenye mchezo wa mwisho wa ligi ya Vodacom msimu uliopita,”amesema Lucas. Lucas amesema Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji bado haijaketi na kutoa maamuzi hivyo mchezaji huyo ataendelea kuwa nje hadi hapo hukumu yake itakapotoka. Amesema kama kufikia Jumamosi Kamati hiyo itakuwa haijakutana na ...