KUNA PRESHA KUBWA KUCHEZA YANGA KULIKO AZAM

Hivi karibuni Gadiel, alijiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Azam ambako alianzia maisha ya soka la ushindani. 
 
BEKI mpya wa Yanga Gadiel Michael, amesema kuna tofauti kubwa kucheza Yanga na klabu nyingine ndogo ambazo hazina presha kama ilivyokuwa Azam FC.

Gadiel, amesema maisha ya Yanga ni mazuri lakini kitu kikubwa kinacho mzingua ni presha ya mashabiki ambao kila mechi wanahitaji mchezaji acheze vizuri na timu ipate ushindi.

“Kiukweli nimepata mapokezi mazuri kwa wachezaji na hata benchi la ufundi ispokuwa presha ni kubwa kuliko umri wangu tofauti na ilivyokuwa Azam, ingawa nashukuru nifurahi kuona watu wanaikubali kazi yangu,”amesema Gadiel.

Beki huyo amesema kitu cha msingi kwake ni kuendelea kucheza kwa kujituma ili kubaki kwenye kikosi cha kwanza vinginevyo anaweza kusota benchi kwani hata msaidizi wake Hajji Mwinyi ni mchezaji mzuri na anaukubali uwezo aliokuwa nao.

Amesema atajitahidi kupambana bila uoga ili kuwaridhisha kocha, mashabiki na viongoi wa timu hiyo pamoja na ushindani ligi ya msimu huu kuwa mkali tofauti na misimu iliyopita nyuma.

Gadiel mbali na uwezo aliokuwa nao wa kuzuia pia beki huyo ameonyesha uwezo mkubwa wa kupanda mbele kusaidia mashambulizi kwa kupiga krosi ambazo zimekuwa zikitumiwa vizuri na washambuliaji wake.

Hivi karibuni Gadiel, alijiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Azam ambako alianzia maisha ya soka la ushindani.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA ILIVYONUSURIKA KUSHUKA DARAJA MWAKA 1989

TUJIKUMBUSHE MECHI KALI KATI YA YANGA NA SIMBA NYAMAGANA 1974?

JINSI YANGA ILIVYOIADHIBU SIMBA MWAKA 1994