YANGA KUKAMILISHA USAJILI BAAB KUBWA WIKI HII
![]() |
| IBRAHIM AJIB |
NA MARIAMU MTORO
Yanga inaendelea na usajili wa wachezaji wapya kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara pamoja na mashindano ya Kimataifa.Habari toka ndani ya timu hiyo zinadai kuwa timu hiyo imepania kufanya vizuri katika mashindano yote itakayoshiriki msimu ujao.Ndo maana wanajitahidi kufanya usajili wa maana kwa kutafuta wachezaji watakaowafaa kitaifa na kimataifa msimu ujao.
Mara baada ya kuwasajili wachezaji kadhaa wakiwemo Ibrahim Ajib toka simba amabaye alifuatiwa na gharama ya kumpoteza kiungo wao mahiri Haruna Niyonzima aliyetimkia Simba,Benedictor Tinocco toka Kagera Sugar,Mwinyi Haji toka KMKM'Vincent Bossou toka{ Togo},Thaban Kamusoko na Donald Ngoma wote platinum zimbabwe,Godfery Mwashiyua Kimondo na Deus Kaseka { Mbeya City}, Antony Mateo Simon, Mudathir Khamis {wote wa KMKM} na Malimi Busungu {Mgambo Jkt},Ndipo Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya timu hiyo,Hussein Nyika ,akaibuka nakuwaahidii mashabiki na vipenzi vya timu hyo kuwa kuna usajili mkubwa utakaotikisa nchi utakaokamilika ndani ya wiki hii
Nyika amesema kuwa usaijili huo unalenga zaidi wachezaji wa kushindana kimataifa na ndio anachokusudia kikamilike katika wikendii hii

Comments
Post a Comment