UPINZANI HAKUNA UCHAGUZI WA TFF.
Arusha. Katibu mkuu wa zamani wa Chama cha Soka Mkoa wa Arusha (ARFA), Adam Brown ameeleza kuwa uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania unaotarajia kufanyika mwezi ujao Dodoma utakuwa rahisi kuliko miaka iliyopita.
Mkongwe huyo aliyewahi kuwa meneja wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ mwaka 2001, alisema hali hiyo ni kutokana na wengi wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi TFF hawajaweka mizizi kwa kiasi kikubwa kwenye familia ya wanamichezo kama ilivyokuwa kwa wagombea wa miaka ya nyuma.
Alisema miaka ya nyuma mtu mwenye nia ya kuwa kiongozi katika shirikisho hilo alikuwa anatambulika mapema kwa matendo yake ya kujihusisha na masuala ya maendeleo ya soka kuanzia mikoani hadi taifa.

Comments
Post a Comment