BUKU TATU KUMUONA ROONEY UWANJA WA TAIFA

                 
                         
       MASHABIKI  wa soka wa Tanzania watapata nafasi ya kumtazama mshambuliaji mpya wa Everton, Wayne Rooney akiongoza timu hiyo dhidi ya Gor Mahia kwa kiingilio cha Sh 3000 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Everton itawasili nchini kesho asubuhi wakata mabingwa wa Kombe la SportPesa, Gor Mahia ya Kenya imewasili leo mchana tayari kwa mchezo huo Alhamisi.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema kiingilio cha chini kitakuwa sh 3000 wakati VIP C itakuwa  sh 8000 na VIP  A na B  kutakuwa na utaratibu maalumu.
Meneja miradi wa kampuni ya Selcom, Gallus Runyeta alisema tiketi zitaanza kuuzwa leo, Jumanne kwa njia ya mtandao, pia mawakala wao watakuwepo Alhamisi siku ya mchezo wakiuza tiketi nje ya uwanja.
Pia, Lucas aliwataja waamuzi watakaochezesha mchezo huo kuwa ni Israel Nkongo atasaidiana na Ferdnand Chacha na  Frank Komba wakati mwamuzi wa akiba atakuwa ni Elly Sasii huku kamishna wa mchezo akiwa ni  Michael Wambura.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA ILIVYONUSURIKA KUSHUKA DARAJA MWAKA 1989

TUJIKUMBUSHE MECHI KALI KATI YA YANGA NA SIMBA NYAMAGANA 1974?

JINSI YANGA ILIVYOIADHIBU SIMBA MWAKA 1994