TASMA (Uchaguzi wa chama cha wataalamu wa Tiba za Michezo),YAWEKA WAZI MAJINA YA WALOCHUKUWA FOMU
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya chama hicho, Leslie Liunda alisema wanaowania uenyekiti ni Joakim Mshanga, Usubene Kisongo na Biyondo Mgome ilihali kwenye nafasi ya Makamu Mwenyekiti, amejitokeza Magreth Mtaki pekee.
anaotaka ukatibu mkuu wa chama hicho ni Suphian Juma na Nassoro Matuzya waliojitokeza huku nafasi ya ukatibu msaidizi inawaniwa na Alfred Mchinamnamba.
Nafasi Mweka Hazina inawaniwa Alex Gongwa huku Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF inawaniwa Richard Yomba na Cosmas Kapinga ilihali Ujumbe wa Kamati ya Utendaji wamo Paschal Itonge na Mwanandi Mwankemwa.
Kwa mujibu wa ratiba ya mchakato wa uchaguzi huo kuanza leo na kesho (Julai 18, 2017 na Julai 19, mwaka huu) watapokea pingamizi katika ofisi za Omlipiki Maalumu (Special Olympic) zilizopo jirani na Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kipindi cha usaili kimepangwa kuanza Julai 20, 2017 hivyo wagombea wote wanatakiwa kufika mbele ya kamati ili kusailiwa.
“Mgombea ambaye atashindwa kuhudhuria atakuwa amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi utafanyika Agosti 5, mwaka huu katika Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam,”

Comments
Post a Comment