SINGIDA UNITED YAKANA KUTAKA KUSAJILI WACHEZAJI TOKA YANGA


DIDA NA BARTHEZ
NA MARIAMU MTORO

Klabu ya Singida United, imesema haina mpango wa kuwasajili wachezaji watatu kutoka Yanga kama inavyodaiwa.
Singida United iliyopanda Ligi Kuu msimu uliopita inahusishwa na kutaka kuwasajili makipa wawili wa Yanga, Deogratius Munishi 'Dida’ na Ally Mustapha ‘Barthez’ pamoja na beki Oscar Joshua.
Katibu mkuu wa Singida United, Abuurahman Sima amekana taarifa hizo kwa kusema timu hiyo haina mpango na wachezaji hao. 
“Hizo ni tetesi tu ambazo ni wakati wake ila kwenye uongozi wetu bado hakuna taarifa za timu yetu kumtaka huyo beki {Joshua} wala kipa yeyote kutoka Yanga kwa wakati huu,” alisema Sima.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA ILIVYONUSURIKA KUSHUKA DARAJA MWAKA 1989

TUJIKUMBUSHE MECHI KALI KATI YA YANGA NA SIMBA NYAMAGANA 1974?

JINSI YANGA ILIVYOIADHIBU SIMBA MWAKA 1994