JULAI 13 EVERTON YAWALETEA UTAMU MASHABIKI WA YANGA
Jaro ambaye ni kivutio cha aina yake, amesisitiza kwamba watatua kwa mamia ndani ya Dar es Salaam na kwa kile wanachokiona kwenye mazoezi ya timu hiyo mjini Nairobi, mashabiki wategemee soka la maana.
Everton, waliomaliza nafasi ya saba kwenye jedwali msimu ulioisha wa Ligi Kuu England, wameanza kuipigia debe mechi hii hadi kiungo wao mahiri Morgan Schneiderlin akaamua kushuhudia mazingira yenyewe alipofika kwa fungate na kipenzie Camille.
“Kwetu si mechi ya kirafiki tu. Huenda mchezaji wetu mmoja au wawili wakaskautiwa na Everton afu pia, kibiashara tunaweza kuanzisha uhusiano wa kipekee. Ni mechi ambayo tunataka ifaidishe Gor Mahia kisoka,” alisema Meneja Jolawi Obondo.
“Kumbuka pia tunawakilisha taifa la Kenya hivyo lazima tusake matokeo mazuri. Tunataka ushindi kuinua bendera ya Kenya. Ni karibu karne hivi mara ya mwisho Gor kucheza na timu ya England wakati huo wakichuana na Norwich City, Kogalo ikiwa chini ya kocha Mwingereza Len Juliens. Tunajua wataleta kikosi chao cha kwanza, hatuna uoga wowote kwani tunapiga mazoezi vilivyo ili tuweze kuwakabili.”

Comments
Post a Comment